Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order, 1967

Government Notice 436 of 1967


Tanzania
Judicature and Application of Laws Act

Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order, 1967

Government Notice 436 of 1967

  • Published in Tanzania Government Gazette
  • Commenced on 1 October 1963
  • [This is the version of this document at 31 July 2002.]
  • [Note: This legislation has been thoroughly revised and consolidated under the supervision of the Attorney General's Office, in compliance with the Laws Revision Act No. 7 of 1994, the Revised Laws and Annual Revision Act (Chapter 356 (R.L.)), and the Interpretation of Laws and General Clauses Act No. 30 of 1972. This version is up-to-date as at 31st July 2002.]
[G.N.s Nos. 436 of 1967; 219 of 1967]

1.

This Order may be cited as the Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order

2.

The declarations set out in the First, Second and Third Schedules to this Order are hereby directed to be the local customary law in respect of the subjects contained therein in the areas subject to the jurisdiction of the Chunya, Dodoma, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Kondoa Manyoni, Maswa, Mbeya, Mpwapwa, Ngara, Njombe, Shinyanga, Singida, Songea, Ufipa, Ukerewe and Pangani District Councils.

First Schedule

Sheria za ulinzi

(1)Ulinzi huwa wa namna hizi zifuatazo:
(a)ulinzi wa watoto waliofiwa na baba wakati wadogo;
(b)ulinzi wa mrithi ambaye hayupo wakati wa kurithi;
(c)ulinzi wa mtu ambaye hawezi kujitegemea kwa sababu ya umaskini au wazimu;
(d)ulinzi wa mke na mtoto wa mtu anayekwenda safari ndefu.

Ulinzi wa watoto:

(2)Mlinzi wa watoto wadogo walifiwa na baba atawekwa na baraza la ukoo.
(3)Ikiwa mtoto wa kiume wa kwanza ni mtu mzima, ndiye atakayewekwa kuwa mlinzi wa watoto wadogo wenzake akiwa yeye ni mwenye akilina ana tabia nzuri.
(4)Ikiwa mtoto wa kiume wa kwanza hafai, atawekwa ndugu mwingine wa ukoo wa marehemu.
(5)Kama baba aliyekufa alikuwa na wake wengi, kila mtoto wa kiume wa kwanza (akiwa ni mtu mzima na akifaa) toka kila nyumba, atafikiriwa kwanza kuwa mlinzi wa wadogo zake katika nyumba yake.
(6)Mlinzi anapowekwa huelezwa na baraza la ukoo wajibu wake wa ulinzi. Kama hakuelezwa, ni juu yake kupata maelezo ya wajibu wake toka baraza la ukoo.
(7)Mama mjane akikubali kurithiwa na ndugu mmoja wa marehemu na amekubaliwa na baraza la ukoo, yeye ndugu ndiye atakayekuwa mlinzi wa watoto wa marehemu.
(8)Ikiwa mlinzi hatimizi wajibu wake, baraza la ukoo lina uwezo wa kumwondoa na kuweka mwingine badala yake, kwa kufuata madai ya mama au ya ndugu yeyote wa ukoo wa kiume.
(9)Mlinzi hawezi kuuza ardhi wala mimea ya daima iliyo chini ya ulinzi wake.
(10)Mlinzi hapati mshahara au malipo maalum kwa kazi yake ya ulinzi, lakini kwa kawaida hukaribishwa kwa vyakula na vinywaji.
(11)Kazi ya mlinzi ni kuwatunza watoto na mama yao, na kuangalia mali yao isipotee wala isiharibike.
(12)Mlinzi ana wajibu wa kuongoza kazi ya kilimo, lakini ashauriane na mama ikiwa yupo nyumbani kwa watoto.
(13)Mlinzi anaweza kumwoza mtoto wa kike, lakini katika shauri hili kwanza akubaliane na mama.
(14)Mlinzi atashughulika na mambo yote ya nje yanayohusu nyumba ile, kwa mfano: kusimamia mashauri, malipo ya kodi na ushuru, ada ya shule, kuhudhuria minada ya mifugo, n.k.
(15)Mlinzi ana wajibu kuangalia mali ya watoto walio chini ya ulinzi wake, bila kuichanganya na mali yake: yaani, mali ya watoto lazima yajulikane kwazi.
(16)Mazao ya mashambani yatatumika nyumbani kwa manufaa ya watu wa nyumbani.
(17)Mazao ya mifugo kama maziwa na samli yatatumika vile vile nyumbani kwa manufaa ya watu wa nyumbani.
(18)Wanyama watakaozaliwa na mifugo pia ni mali ya watoto.
(19)Mlinzi anaweza kuchinja, kuuza au kubadilisha wanyama kwa faida au mahitaji ya nyumbani.
(20)Kama marehemu alikuwa na wake wawili au zaidi, na hakuna mjane aliyekubali kurithiwa, baraza la ukoo linaweza kuweka mlinzi mmoja kwa nyumba zote.
(21)Mashtaka au madai juu ya ulinzi yanaweza kuletwa na mama wa watoto, ndugu mwingine, na hata na watoto wenyewe watakapokua.
(22)Mashauri kama haya yasipokelewe na baraza la hakimu ikiwa hayakufikishwa kwanza kwa baraza la ukoo.
(23)Mlinzi akifa, atawekwa mwingine na baraza la ukoo.
(24)Mrithi wa kwanza atakapofikia umri wa miaka 21 au atakapooa (akioa kabla ya kufikia umri huu) na akifaa, anawekwa na baraza la ukoo kuwa mlinzi wa watoto wadogo wenzake.
(25)Watoto wengine wengine vile vile watatoka katika ulinzi wakapofikia umri wa miaka 21 au watakapooa au kuolewa.
(26)Ikiwa hayupo ndugu yeyote wa ukoo wa watoto, baraza la ukoo wa mama litaweka mlinzi waukoo wake.
(27)Ikiwa hakuna ndugu kabisa, baraza la hakimu kufuata maombi ya mtu yeyote linaweza kuweka mtu baki kuwa mlinzi wa watoto.

Ulinzi wa mrithi asiyekuwapo:

(28)Ikiwa mmoja wa warithi hayupo wakati wa kurithi, ndugu mwingine wa ukoo wake huwekwa kuangalia mali mpaka mrithi atakaporudi.
(29)Mlinzi wa mrithi asiyekuwapo anawekwa na baraza la ukoo, na anapowekwa huelezwa na baraza la ukoo wajibu wake wa ulinzi. Kama hakuelezwa, ni juu yake kupata maelezo ya wajibu wake toka baraza la ukoo.
(30)Mkubwa kati ya warithi waliopo atafikiriwa kwanza na baraza la ukoo, na ikiwa kwa maoni yao ni mwenye akili ya kutosha na ana tabia nzuri, yeye ndiye atakayewekwa kuwa mlinzi wa mrithi asiyekuwapo.
(31)Ikiwa warithi wote hawapo baraa la ukoo litaweka mlinzi mmoja wa ukoo ule kuangalia mali yote ya urithi.
(32)Mlinzi wa marithi asiyekuwapo akipoteza au akiharibu mali ya mrithi anaweza kudaiwa.
(33)Mlinzi hawezi kuchanganya mali ya urithi pamoja na mali yake: yaani, mali ya mrithi lazima yajulikane wazi.
(34)Mlinzi hawezi kutumia mwenyewe mali ya mrithi asiyokuwapo.
(35)Mazao ya mali ya mrithi asiyekuwapo yanaweza kuuzwa kwa shida za nyumbani kwa mrithi: yakiuzwa kwa wingi ni mali ya mrithi.
(36)Mlinzi wa mrithi asiyekuwapo hapati mashahra wu malipo maalum kwa kazi anayofanya.
(37)Baraza la ukoo linaweza kumwondoa mlinzi ikiwa hatimizi wajibu wake, na kuweka mwingine, kwa kufuata madai au mashaka ya ndugu yeyote wa mrithi asiyekuwapo.
(38)Ikiwa hayupo mtu yeyote wa ukoo wa mrithi asiyekuwapo, baraza la hakimu kufuata taarifa ya mtu yeyote linaweza kuweka mtu baki kuwa mlinzi kwa mpango unayofaa.

Ulinzi wa mtu ambaye hawezi kujitegemea:

(39)Mtu ambaye hawezi kujitegemea kwa sababu ya umaskini au wazimu huwekwa chini ya ulinzi wa mtu wa ukoo wake.
(40)Mlinzi huyu anawekwa na baraza la ukoo, na wajibu wake ni sawa kama wa mlinzi wa mtoto.
(41)Kama mtu ambaye hawezi kujitegemea kwea sababu ya umaskini au wazimu huwekwa chini ya ulinzi wa mtu wa ukoo wake.

Ulinzi wa jamaa na mali ya mtu anayesafiri:

(42)Ikiwa mume anaondoka kwa safari ndefu, anaweza kuchagua mlinzi kuangalia mkewe, watoto na mali yake.
(43)Mlinzi atasimamia mifugo na kilimo.
(44)Mlinzi ataangalia mambo yote ya nje yanayohusu nyumba ile, ambayo yangaliangaliwa na mume mwenyewe.
(45)Mlinzi atashughulika na shida zote za watu wa nyumbani kwa msafiri.
(46)Mke hawezi kuhama toka mji wa mume wake bila ruhusa ya mlinzi.
(47)Mke wa msafiri anaweza kufumaniwa na mlinzi.
(48)Mlinzi anaweza kufungua shauri la ugoni barazani badala ya mume.
(49)Ni mume tu anayeweza kumwondoa mlinzi.
(50)Mlinzi aiifa au akihama kabisa na mume hawezi kuarifiwa, baraza la ukoo linaweza kuweka mlinzi mwingine.
(51)Mlinzi hawezi kudai cho chote kwa kazi yake ya ulinzi.
(52)Mlinzi akikosa katika wajibu wake wa kuangalia mali ya msafiri na kutunza mkewe na watoto wake, anaweza kuitwa na kuonyea na bareaza la ukoo.
(53)Akiendelea na makosa yake, mlinzi anaweza kuitwa shaurini na mke au ndugu yeyote wa msafiri katika bareaza la hakimu.

Second Schedule

Sheria za urithi

(1)Urithi hufuata upande wa ukoo wa kiume.
(2)Asimamiaye mazishi ni kaka wa marehemu aliye mkubwa au, kama hakuna kaka ndugu mwingine wa kiume ailiye karibu.
(3)Ikiwa marehemu alikuwa mtoto, msimamizi ni babaye au mlinzi wake.
(4)Matumizi ya mazishi na matanga hutoka katika mali ya marehemu, lakini ikiwa marehemu hakuacha mali, hushughulika msimamizi.
(5)Msimamizi wa kugawanya urithini kaka wa marehemu aliye mkubwa, au babaye, na kama kaka au baba hakuna, ni ndugu wa kiume mwingine akisaidiwa na baraza la ukoo. Kama hakuna ndugu wa kiume, asimamie ndugu wa kike.
(6)Baada ya matanga watu wa ukoo hukusanyika na wanahesabu urithi na kushauriana juu ya madai na madeni yote aliyokuwa nayo marehemu.
(7)Wenye kudai huitwa na hutaja madai yao.
(8)Wadeni wa marehemu hutangaziwa vile vile na utaratibu wa kulipa hutengenezwa.
(9)Baada ya hesabu madeni na madai, mpango wa kugawanya urithi unakubaliwa.
(10)Ikiwa mdai ye yote hataji madai yake akiwepo katika mkutano, madai yake hayapokelewi baadaye.
(11)Ikiwa mali ya urithi haitoshi kulipa madeni yote ya marehemu, madeni ya muhimu hulipwa kwanza na madeni mengine yanalipwa kwa sehemu kadiri iwezekanavyo.
(12)Baki ya madeni humalizwa na warithi toka mali yao wenyewe.
(13)Madai na madeni ya marehemu hurithiwa.
(14)Baada ya mpango kutengenezwa, mali ya urithi kwa kawaida hugawanyiwa upesi.
(15)Kama hakuna matatizo, mgawanyo wa mali unafanyiwa katika siku chache baada ya matanga na kwa vyo vyote muda hauzidi mwezi mmoja.
(16)Kama mrithi mmoja anataka kuchukua sehemu yake, mgawanyo hufanyiwa mara.
(17)Kama warithi wote hawana haraka hakuna lazima ya kugawanya upesi.
(18)Ikiwa wadai wengine hawakuwepo au hawakupata habari wakati wa matanga, watamdai mrithi wa kwanza, na ikiwa urithi umekwisha gawanyiwa, mrithi wa kwanza atasaidiwa kuwalipa na warithi wenzake kadiri ya sehemu ya urithi waliyopata.
(19)Mrithi wa kwanza wa marehemu ni mtoto wa kiume wa kwanza toka nyumba ya kwanza. kama marehemu hakuacha mtoto wa kiume katika nyumba ya kwanza, mtoto wake wa kiume aliyezaliwa kwanza toka nyumba yoyote atakuwa mrithi wa kwanza.
(20)Wanawake wanaweza kurithi, isipokuwa ardhi ya ukoo, ambayo wanaweza kuitumia bila kuiuza wakati wa uhai wao. Lakini, kama hakuna wanamume wa ukoo ule, wanamke anaweza kurithi ardhi hii kabisa.
(21)Urithi una vyeo vitatu: cheo cha kwanza, cheo cha pili na cheo cha tatu.
(22)Mwenye cheo cha kwanza ni mrithi wa kwanza na yeye anapata sehemu iliyo kubwa ya urithi kupita sehemu yo yote ya warithi wenzake.
(23)Wenye cheo cha pili watapata kila mmoja sehemu ya urithi iliyo kubwa kuliko sehemu ya wale walio katika cheo cha tatu.
(24)Ikiwa marehemu amewagawia warithi wake sehemu ya mali yake wakati alipokuwa bado hai, sehemu hii inahesabiwa katika mgawanyo wa mali baada ya kifo chake.
(25)Kwa kawaida, cheo cha kwanza ni cha mtoto wa kiume wa kwanza, cheo cha pili ni cha watoto wa kiume wengine, na cheo cha tatu ni cha watoto wa kike.
(26)Kama marehemu ameacha watoto wa kiume, au wa kiume pamoja na wa kike, hao ndio watakaorithi mali yake yote.
(27)Mjane hana fungu lake katika urithi ikiwa marehemu aliacha jamaa na ukoo wake: fungu lake in kutunzwa na watoto wake, jinsi alivyowatunza. (Fungu la mjane mgumba lililotajwa katika kifungu 77, Sheria zinazohusu Hali ya Watu1, halihesabiwi katika urithi wa mumewe).1First Schedule to G.N. No. 279 of 1963
(28)Mume hawezi kurithi mali ya mke ake katika urithi usio na wosia-ila kama mke hakuacha watoto na hakuacha kabisa mtu yeyote wa ukoo wake.
(29)Kama hakuna watoto wa kiume, mtoto wa kike mkubwa toka nyumba ya kwanza ni mrithi wa kwanza. Ila, kama kuna ndugu wa kiume, yule ndugu aliye badala ya baba ndiye atakayepokea mahari ya watoto wa kike watakapoolewa.
(30)Utaraibu wa mgawayo wa urithi kati ya warithi wa cheo cha pili na cha tatu hufuatana na umri wao-yaani, wakubwa watapata zaidi ya wadogo na wa kiume wapate zaidi ya wa kike.MFANO-Urithi uliyokuwa wa ng'ombe peke yake:Jumla ya ng'ombe 24.Cheo I - Mtoto wa kiume - Umri 23-atapata ng'ombe 9.Cheo II - Mtoto wa kiume - Umri 20-atapata ng'ombe 5.Mtoto wa kiume - Umri 14-atapata ng'ombe 4.Cheo III - Mtoto wa kike - Umri 25-atapata ng'ombe 3.Mtoto wa kike - Umri 22-atapata ng'ombe 2.Mtoto wa kike - Umri 18-atapata ng'ombe 1.
(31)Kama mtoto ni mmoja tu peke yake, yeye atarithi mali yote-isipokuwa kama yeye ni mwanamke hawezi kurithi ardhi ya ukoo, ambayo ataweza kuitumia bila kuiza wakati wa uhai wake. Hata hivyo, kifungu cha 20 kifuatwe.
(32)Ikiwa watoto wa kike wapo, ila hakuna watoto wa kiume walio hai au walioacha watoto wao, hakuna cheo cha pili.
(33)Ikiwa watoto wa kiume wapo, ila hakuna watoto wa kike walio hai au walioacha watoto wenyewe, hakuna chao cha tatu.
(34)Wajukuu watarithi cheo cha baba au mama yao katika urithi wa babu ikiwa baba au mama yao amekufa kabla ya babu.
(35)Lakini kama wajukuu ni watoto wa mtoto wa kiume wa kwanza, wao hawatapata cheo cha kwanza ikiwa babu yao aliacha mtoto wa kiume mwingine toka nyumba ile.
(36)Ikiwa ni hivyo, mtoto wa kiume mkubwa aliyebaki ndiye atakayekuwa mrithi wa kwanza, na atakayepata cheo cha kwanza katika urithi wa babaye.
(37)Wajukuu wale halafu watatangulia katika cheo cha pili.
(38)Mtoto asiye halai (yaani, aliyekwenda ujombani) atarithi katika urithi wa mama yake; na kama mama yake alikufa bila kuacha watoto halali na kabla ya babu, mtoto huyu asiye halai atarithi cheo cha mama katika urithi wa babu.
(39)Kama mama wa mtoto asiye halali hakuwa na mtoto mwingine isipokuwa mama wa mtoto huyu na kama mama amekufa, mtoto huyu asiye halali atakuwa mrithi halali wa babu yake.
(40)Kama babu wa mtoto asiye halali hakuwa na mtoto mwingine isipokuwa maam wa mtoto huyu na kama mama yake kwa kufuata umri wake pamoja na watoto wale wengine.
(41)Watoto waliohalalishwa kwa ndoa ya wazazi wao wanahesabiwa kama watoto walizaliwa halali, isipokuwa mtoto aliyehalalishwa kwa ndoa hawezi kutangulia katika urithi ingawa alizaliwa kwanza, ikiwa kuna mtoto wa kiume mwingine wa nyumba ingine ambaye mama yake aliolewa na marehemu kabla ya mama wa mtoto aliyehalalishwa.
(42)Watoto waliohalilishwa kwa malipo maalum (yaliyotajwa katika kifungu 181 cha Sheria zinazohusu Hali ya Watu)2 watarithi nyuma ya watoto waliozaliwa na katika cheo cha pili kama ni mwanamume na katika cheo cha tatu kama ni mwanamke.2First Schedule to G.N. No. 279 of 1963
(43)Watoto wasio halali hawawezi kurithi upande wa kiume katika urithi usio na wosia.
(44)Ikiwa marehemu hakuacha watoto wala wajukuu, watarithi kaka na dada zake waliochangia bab na mama-kaka wa kwanza atakuwa na cheo cha kwanza, kaka mwingine na cheo cha pili na dada cheo cha tatu.
(45)Ikiwa marehemu hakuacha kaka wala dada waliochangia baba na mama, watoto wa kaka au dada waliochangia baba na mama watarithi mali ya marehemu huyo kabla ya kaka au dada wa kuumeni, yaani wa baba mmoja ila mama mbali mbali.
(46)Ikiwa hakuna kaka au dada wowote, watarithi watoto wao.
(47)Ikiwa marehemu hakuacha kaka au dada wala watoto wao, atarithi babaye.
(48)Ikiwa baba mzazi amekwisha kufa, watarithi baba wadogo na shangazi.
(49)Ikiwa hakuna baba au shangazi, watarithi ndugu wengine wa kuumeni.
(50)Ikiwa hakuna ndugu kabisa, mume atarithi mali ya mke, na mke atarithi mali ya mumewe.
(51)Warithi au mrithi wa mume watakuwa na wajibu wa kumtunza mjane.
(52)Kama hakuna mrithi, mali ya marehemu itachukuliwa na Serikali ya Mtaa.
(53)Mkuu wa ukoo akifa, mkuu mpya huchaguliwa na baraza la ukoo.

Third Schedule

Sheria za wosia

(1)Wosia maana yake ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonyesha nia yake jinsi gani angependa mali yake ingawanye baada ya kufa kwake.
(2)Wosia unaweza kuwa wa namna bili; wosia wa mdomo na wosia uliyoandikwa.
(3)Wosia uhsuhudiwe na mashahidi maalum ambao lazima wawepo wakati mmoja.
(4)Mashahidi hawa huchaguliwa na mwenye kutoa wosia mwenyewe.
(5)Zaidi ya mashahidi maalum, mkewe (mwenyewe kutoa wosia) au wake zake waliopo nyumbani lazima washuhudie vile vile.
(6)Watu wanaorithi kitu ch chote kutoka wosia hawawezi kuhesabiwa kama mashahidi kushuhudia wosia ule-isipokuwa mke au wake wa mwenye kutoa wosia.
(7)Wosia hauna nguvu ikiwa mwenye kutoa wosia amepungukiwa akili kwa sababu ya wazimu, ugonjwa, ulevi au hasira ya ghafula.
(8)Wosia hauwezi kupingwa kwa sababu hizi, isipokuwa na mtu anayehusika.
(9)Kama mwenye kutoa wosia alikuwa na akili ya kutosha itategemea ushahidi wa wale mashahidi maalum na wa mke wake au wake zake, na hata ushahidi mwingine kama upo.
(10)Kama mashahidi hawapatani, itakuwa juu ya baraza kupima na kukubali ushahidi utakaofaa.Wosia wa mdomo:
(11)Wosia wa mdomo ushuhudiwe na mashahidi wasiopungua wanne-yaani, watu wa ukoo wasipungue wawili na watu baki wasipungue wawili.
(12)Wosia wa mdomo unaweza kubadilishwa au kufutwa kwa kufuata ule utaratibu uliyoelezwa katika vifungu vya 4, 5, na 11.
(13)Mashahidi wa wosia wa kwanza, ikiwa wapo na wanaweza kupatikana, washuhudie.
(14)Ikiwa mashahidi wamekufa wote kabla ya mwenye kutoa wosia hajafa, wosia hauwezi kukubaliwa, na urithi utagawanyika kufuata mpango wa urithi usio na wosia.
(15)Mwenyewe kama anataka kuusia mali yake, lazima atoe wosia mpya.
(16)Ikiwa mashahidi wengine wamekufa, lakini walio hai bado hawapungui wawili, wosia utafuatwa.

Wosia wa kuandika:

(17)Wosia wa kuandika usiandikwe na kalamu ya risasi: unaweza kupigwa chapa au kuandikwa na wino au na kalamu isiyofutika.
(18)Tarehe ya wosia uliyoandikwa lazima iwekwe.
(19)Wosia uliyoandikwa ushuhudiwe na mashahidi wanaojua kusoma na kuandika-yaani mashahidi wasipungue wawili (mmoja wa ukoo na mmoja mtu baki) ikiwa mwenye wosia anajua kusoma na kuandika, na wasipungue wanne Swahili wa ukoo na wawili watu baki)-ikiwa mwenyewe hajui kusoma na kuandika.
(20)Mwenyewe atie sahihi yake katika wosia uliyoandikwa ikiwa anajua kusoma na kuandika: ikiwa haui, aweke alama ya kidole chake cha gumba cha kulia.
(21)Mashahidi washuhudie sahihi au alama ya mwenye kutoa wosia, na wenyewe watie sahihi zao katika wosia.
(22)Karatasi yenye maandiko ya wosia isijazwe wala isiongezwe na mtu ye yote.
(23)Wosia uliyoandikwa unaweza kubadilishwa au kufutwa kwa kutengeneza wosia uliyoandikwa mwingine.
(24)Wosia uliyoandikwa unaweza kuandikishwa au kuwekwa barazani, lakini si lazima ila hiari.
(25)Uandikishaji au uwekaji huu haukubaliwi kuwa uhtibitisho wa wosia ikiwa masharti yote ya sheria yaliotajwa mbele hayakutimizwa.
(26)Mtu aliye chini ya umri wa miaka 21 hawezi kutoa wosia wa mdomo wala wosia uliyoandikwa.
(27)Wosia uliyoandikwa hauwezi kufutwa au kubadilishwa na wosia wa mdomo; lakini wosia wa mdomo unaweza kubadilishwa au kufutwa na wosia uliyoandikwa, wakihudhuria mashahidi wote walio hai na wanaoweza kupatikana walioshuhudia wosia wa mdomo.

Kuhusu wosia za aina zote mbili:

(28)Mwenye kutoa wosia anaweza kuusia mali yake yote bila kutaja kila kitu atakachokuwa nacho wakati wa kufa kwake.
(29)Ikiwa mwenye kutoa wosia anausia sehemu tu ya mali atkayekuwa nayo, baki itagawanywa kufuata masharti ya urithi usio na wosia-isipokuwa kama mtu anayeusiwa angestahili kurithi kufuata mpango wa urithi usio na wosia, mali anayoachiwa katika wosia itahesabiwa wakati wa kugawanywa baki.
(30)Sababu zinazohesabiwa ni nzito za kuwezesha mwenye kutoa wosia kumnyima marithi usio na wosia-isipokuwa kama mtu anayeusiwa angestahili kurithi kufuata mpango wa urithi usio na wosia, mali anayoachiwa katika wosia itahesabiwa wakati wa kugawanywa baki.
(31)Sababu zinazohesabiwa ni nzito za kuwezesha mwenye kutoa wosia kumnyima mrithi urithi wake ni hizi zifuatazo:—
(i)Ikiwa mrithi amezini na mke wa mwenye kutoa wosia;
(ii)Ikiwa mrithi amejaribu kumua, amemshambulia au amemdhuru vibaya mwenye kutoa au mama mzazi wake (yaani, wa mrithi);
(iii)Ikiwa mrithi, bila sababu ya haki, hakumtunza mwenye kutoa wosia katika shida ya njaa au ya ugonjwa.
(32)Ikiwa mrithi ameharibu mali ya mwenye kutoa wosia, uharibifu wake utahesabiwa katika kukisia sehemu ya urithi atakayostahili kupata.
(33)Dini haihesabiwi kama sababu ya kumnyima mtu urithi.
(34)Mtu atakaye kumnyima mrithi urithi wake lazima aseme wazi katika wosia wake na aeleze sababu zake.
(35)Mrithi aliyenyimwa urithi wake apate nafasi kujitetea mbele ya mwenye kutoa wosia au mbele ya baraza la ukoo.
(36)Mtu ambaye alijua kwamba amenyimwa urithi na ambaye hakushughulika kujitetea hawezi kupinga wosia baada ya kufa mwenye kutoa wosia.
(37)Ikiwa mtu aliyenyimwa urithi hakuwa na habari kabla ya kifo cha mwenye kutoa wosia, atasikilizwa na baraza la ukoo-litakalokuwa na haki ya kukubali au kukataa madai yake.
(38)Kama inaonekana kwamba mtu amenyimwa urithi katika wosia pasipokuwepo sababu ya haki, wosia unavunjwa na urithi utagawanyiwa kufuata mpango wa urithi usio na wosia.
(39)Shauri kama hili huamuliwa na baraza la ukoo, ila mtu anayehusika asiporidhika anaweza kufika barazani kwa hakimu.
(40)Mume anaweza kumwusia mkewe mazao au mapato ya mali yake mpaka aolewe tena au afe.
(41)Kama mume anao wake wengi anaweza kuwausia watoto (siyo kuwapa wengine na wengine kuwanyima) mazao au mapato ya mali yake kwa kufuata vyeo vya urithi usio na wosia, mpaka waolewe tena au wafe.
(42)Mjane asiye na watoto anaweza kuusiwa hata mazao au mapato ya ile sehemu ya mali aliyochuma na mumewe (na aliyotajwa katika kifungu 77 ya Sheria zinazohusu Hali ya Wat)3 ambayo ingalirudi kuumeni.3First Schedule to G.N. No. 279 of 1963
(43)Mtu anaweza kumrithisha rafiki yake vitu au vyombo vyake alivyokuwa akivitumia mwenyewe binafsi au sehemu ya urithi isiyozidi fungu la kila mrithi halisi.
▲ To the top

History of this document

31 July 2002 this version
Consolidation
01 October 1963
Commenced