Kanuni za Kuratibu Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2023

Government Notice 209 of 2023

Kanuni za Kuratibu Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2023

Tanzania
Political Parties Act

Kanuni za Kuratibu Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2023

Tangazo la Serikali 209 ya 2023

[Zimetengezwa chini ya kifungu cha 22(2)(j)]

Sehemu ya kwanza – Masharti ya utangulizi

1. Jina la Kanuni

Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Kuratibu Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2023.

2. Matumizi

Kanuni hizi zitatumika kwa vyama vya siasa vilivyo na usajili wa muda na usajili kamili, mwanachama wa chama cha siasa na mtu yeyote anayeshiriki katika mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

3. Tafsiri

Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—"chama cha siasa" maana yake ni kikundi chochote kilichoundwa kwa utaratibu maalum kwa madhumuni ya kuunda Serikali au Mamlaka ya Serikali za Mitaa ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa njia ya uchaguzi au kuweka au kuwaunga mkono wagombea katika uchaguzi huo;Katiba” maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977;Msajili” maana yake ni Msajili wa Vyama vya Siasa aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria na inajumuisha Naibu Msajili na Msajili Msaidizi; naSheria” maana yake ni Sheria ya Vyama vya Siasa.[Sura ya 258]

Sehemu ya pili – Utaratibu wa kuendesha mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa

4. Haki ya kufanya mikutano ya hadhara

Kila chama cha siasa kilicho na usajili wa muda au usajili kamili kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya hadhara kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni hizi.

5. Utoaji taarifa

Taarifa ya maandishi ya kufanya mkutano wa hadhara chini ya kifungu cha 11(4) cha Sheria pamoja na masuala yaliyoainishwa kwenye kifungu cha 11(5) cha Sheria, itabainisha yafuatayo:
(a)jina, kitambulisho cha uraia, anwani ya mahali na namba ya simu iliyosajiliwa ya kiongozi wa chama katika eneo husika;
(b)jina la msemaji mkuu katika mkutano; na
(c)mpangilio wa matukio katika mkutano.

6. Masharti ya kuendesha mikutano ya hadhara

Kwa kuzingatia kifungu cha 11 cha Sheria, pale ambapo kibali kitahitajika kwa ajili ya matumizi ya eneo lolote au vifaa kuhusiana na mkutano wa hadhara unaopendekezwa, chama cha siasa kitaomba kibali hicho kwa mamlaka inayohusika kabla ya kufanya mkutano.

7. Muda wa kufanya mikutano ya hadhara

Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa itafanyika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni.

Sehemu ya tatu – Masuala ya kuzingatia wakati wa kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa

8. Mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya mikutano ya hadhara

(1)Chama cha siasa kilichosajiliwa, mwanachama wa chama cha siasa na mtu yeyote anayeshiriki katika mkutano wa hadhara wa chama cha siasa hatatakiwa—
(a)kutamka au, kwa namna nyingine yoyote kutumia lugha ya matusi, vitisho, udhalilishaji, kashfa, maneno ya uchochezi au vurugu kwa mtu yeyote;
(b)kutamka au kutumia maneno yoyote au kufanya jambo lolote ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani, umoja wa kitaifa au maslahi ya taifa;
(c)kujihusisha na kitu chochote ambacho kinaweza kusababisha fujo, vitisho, migogoro au uharibifu wa mali;
(d)kutoa matamko au taarifa zilizozuiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(e)kutoa kauli ambazo zinaweza kusababisha vitisho au hatari kwa shughuli za maendeleo ya nchi au utulivu wa kisiasa;
(f)kunyanyasa au kuzuia waandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yao;
(g)Kus
(h)hawishi au kuchochea wanachama au wafuasi kufanya jambo lolote ambalo limekatazwa na sheria yoyote;
(i)kugombana au, kwa namna nyingine yoyote, kusababisha usumbufu kwa namna ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani; na
(j)kuvaa sare za Jeshi lolote la Ulinzi la Jamhuri ya Muungano au za chombo chochote cha ulinzi kilichowekwa na sheria au vazi lolote lenye mwonekano au lenye alama zozote za kijeshi.

9. Wajibu wa vyama vya siasa katika mikutano ya hadhara

Chama cha siasa kinachoendesha mkutano wa hadhara kitatakiwa—
(a)kuzuia matamshi au kitendo chochote au kauli nyingine yoyote ambayo inaweza kusababisha chuki au ubaguzi kwa misingi ya dini, kabila, jinsia, rangi au aina nyingine yoyote ya ubaguzi;
(b)kuhakikisha wanachama au wafuasi wake hawasababishi kuvunjika kwa mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na vyama vingine; na
(c)kuhakikisha kwamba mkutano wa hadhara wa chama cha siasa hauathiri au kuzuia ufanyaji wa shughuli za maendeleo au shughuli nyingine zozote za kijamii.

10. Wajibu wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi litakuwa na wajibu wa kuhakikisha ulinzi wa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na mtu mwingine yeyote anayeshiriki katika mikutano hiyo.

11. Adhabu

(1)Endapo chama cha siasa kilichosajiliwa au mwanachama wa chama cha siasa anayeshiriki katika mkutano wa hadhara wa chama cha siasa atakiuka masharti yoyote ya Kanuni hizi, Msajili, yeye mwenyewe au baada ya kupokea malalamiko kwa maandishi kutoka kwa mtu yeyote kuhusu ukiukwaji wa Kanuni hizi na kujiridhisha, anaweza kutoa adhabu zifuatazo:
(a)onyo au karipio;
(b)kutoa amri kwa mkosaji au mkiukaji kurekebisha kosa alilofanya;
(c)kuamuru mkosaji au mkiukaji kuomba radhi hadharani kupitia vyombo vya habari vinavyosomwa, kusikilizwa au kutazamwa kwa wingi nchini;
(d)kutangaza hadharani jina la mkosaji au mkiukaji, kueleza ukiukwaji na kumuonya kutorudia ukiukaji huo kupitia vyombo vya habari vinavyosomwa, kusikilizwa au kutazamwa kwa wingi; au
(e)adhabu nyingine yoyote ambayo Msajili anaweza kutoa kwa mujibu wa Sheria.
(2)Kabla ya kutoa adhabu chini ya kanuni ndogo ya (1), Msajili atahakikisha kwamba—
(a)amekijulisha chama kinachohusika na ukiukaji huo kwa maandishi; na
(b)amepokea au ameshindwa kupokea utetezi, ndani ya muda uliowekwa.
▲ To the top

History of this document

17 March 2023 this version