Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Amani ya Mwaka 2023

Government Notice 220 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Amani ya Mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Amani ya Mwaka 2023

Tangazo la Serikali 220 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itaitwa Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Amani ya Mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji (Mpango wa Urasimishaji) kwa madhumuni ya Sheria ya Mipango Miji.[Sura ya 355]

3. Mpango katika eneo la kwenye Jedwali

Mipangoya jumla na kina katika eneo lililoainishwa katika Jedwali itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo:"Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 01 yenye majira - nukta 753530MS, 9083510KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 2.43 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 02 yenye majira - nukta 753772MS, 9083490KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 3.28 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 03 yenye majira - nukta 753872MS, 9083178KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 04 yenye majira - nukta 753891MS, 9083190KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa Kilomita 1.8 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 05 yenye majira - nukta 754071MS, 9083176KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 06 yenye majira - nukta 753977MS, 9082816KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 2.62 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 07 yenye majira - nukta 753741MS, 9082932KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi kwa umbali wa Kilomita 3.70 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 08 yenye majira - nukta 753529MS, 9082232KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea mashariki hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 09 yenye majira - nukta 753553MS, 9083234KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 2.80 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba AM 01 hadi ulipoanzia"
▲ To the top

History of this document

24 March 2023 this version