Amri ya Kupanga Eneo la Babayu ya mwaka, 2023

Government Notice 249 of 2023

Amri ya Kupanga Eneo la Babayu ya mwaka, 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kupanga Eneo la Babayu ya mwaka, 2023

Tangazo la Serikali 249 ya 2023

  • Imechapishwa katika Gazette of the United Republic of Tanzania 10 hadi 24 Machi 2023
  • Imeidhinishwa tarehe 6 Februari 2023
  • Ilianza tarehe 24 Machi 2023
  • [Hili ni toleo la hati hii kutoka 24 Machi 2023.]
  • [Kumbuka: Hati asili ya uchapishaji haipatikani na maudhui haya hayakuweza kuthibitishwa.]
[Imetengenezwa chini ya Kifungu cha 8(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kupanga Eneo la Babayu ya mwaka, 2023

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipango Miji.[sura (355)]

3. Mpango wa jumla na kina wa eneo

Mipango ya jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.

Jedwali (Limeandaliwa chini ya aya ya 2)

Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo:—“Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BY1 yenye majira - nukta 795402.503MS, 9383995.191KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa MS88052’24.06”MS kwa umbali wa kilomita 5.64 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BY2 yenye majira - nukta 801085.510MS, 9384106.954KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa KS9058’22.45” kwa umbali wa kilomita 7.45 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BY3 yenye majira - nukta 799793.143MS, 9376768.661KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi kwa kukatiza barabara ya Dodoma - Babayu katika uelekeo wa KS78042’05.92”MG kwa umbali wa kilomita 13.97 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BY4 yenye majira - nukta 786093.954MS, 9374031.301KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ23051’17.45”MG kwa umbali wa kilomita 8.96 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BY5 yenye majira - nukta 789721.189MS, 9382234.068KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KS65044’59.47”MS kwa umbali wa kilomita 2.96 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BY6 yenye majira - nukta 792422.141MS, 9381017.370MG; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ45001’27.93”MG kwa umbali wa kilomita 4.21 hadi ulipoanzia.”
▲ To the top

History of this document

24 March 2023 this version
Published in Gazette of the United Republic of Tanzania 10
Commenced
06 February 2023
Assented to