Amri ya Tozo za Wakusanyaji na Watawanyaji wa Mizigo ya Mwaka 2023

Government Notice 269 of 2023

Amri ya Tozo za Wakusanyaji na Watawanyaji wa Mizigo ya Mwaka 2023

Tanzania

Amri ya Tozo za Wakusanyaji na Watawanyaji wa Mizigo ya Mwaka 2023

Tangazo la Serikali 269 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 28(3)]

Sehemu ya kwanza – Masharti ya awali

1. Jina na tarehe ya kuanza kutumika

Amri hii itajulikana kama Amri ya Tozo za Wakusanyaji na Watawanyaji wa Mizigo ya Mwaka 2023 na itaanza kutumika siku kumi na nne kuanzia tarehe ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.

2. Matumizi

Amri hii itatumika kwa wakusanyaji na watawanyaji wa mizigo waliopewa leseni kwa mujibu wa Sheria.

3. Tafsiri

Katika Amri hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo:hati ndogo ya mzigo majini” maana yake ni nyaraka ya usafirishaji ya mzigo iliyotolewa na mkusanyaji mzigo kwa mtumaji wa mzigo ikionesha hati ya mzigo uliokusanywa ikiwa na taarifa za uzito wa mzigo, vipimo, maelezo ya mzigo na idadi, jina la mtumaji na mpokeaji, jina la meli, bandari iliyopakia mizogo na bandari itakayoshusha mzigo na namba ya hati ya mzigo majini;[TS. Na. 337 la 2018]hati ya kukabidhi” maana yake ni nyaraka inayotolewa na mtawanyaji wa mzigo, kwa niaba ya mkusanyaji wa mzigo, kwa mtu aliyetajwa ikiidhinisha mwendeshaji wa bandari au bandari kavu kukabidhi mzigo ulio katika hati ndogo ya mzigo majini kwa mtu aliyetajwa;mpokeaji wa mzigo” maana yake ni mtu ambaye anatumiwa mzigo uliopokelewa kubebwa kwenye meli na ambaye ametajwa hivyo kwenye hati ndogo ya mzigo majini;mtumaji” maana yake ni mtumaji wa mzigo aliyetajwa katika hati ndogo ya mzigo majini ambaye anawajibika kuanzisha mchakato wa kusafirisha, na ambaye anawajibika kulipia gharama za usafirishaji au kuingia mkataba na msafirishaji kuhusu namna gharama za usafirishaji zitakavyolipwa;Sheria” maana yake ni Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania;[Sura ya 415]Shirika” maana yake Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lilioanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria;tozo” maana yake ni gharama au bei pamoja na vigezo na masharti yanayotumiwa na mtoa huduma anayedhibitiwa;[TS. Na. 7 la 2020]ukusanyaji wa mizigo” maana yake ni kuunganisha mizigo miwili au zaidi kutoka kwa watumaji wa mzigo na kufanya mzigo mmoja kwa ajili ya usafirishaji katika meli, au katika kasha moja na unaweza kujumuisha uratibu wa kazi za upokeaji mizigo, kuhifadhi, kuipanga, kuiandaa kwa kutumwa, kuiwekea utambulisho na alama kama itakavyolazimu katika ukusanyaji wa mizigo;[TS. Na. 3 37 la 2018]utawanyaji wa mizigo” maana yake kutenganisha mzigo ulio katika hati ya mzigo majini katika mizigo miwili au zaidi kwa mujibu wa hati ndogo za mzigo majini kwa ajili ya kukabidhi kwa wapokeaji na unaweza kuhusisha uratibu wa kazi ya kuhifadhi mzigo, kufungua mzigo na kupanga kama itakavyolazimu katika kutenganisha na kukabidhi mzigo kwa wamiliki;wakala wa meli” maana yake ni kampuni inayojihusisha na utoaji wa huduma za uwakala wa meli katika bandari za bahari kwa mujibu wa Sheria.

Sehemu ya pili – Tozo na masharti yanayotumiwa

4. Tozo zilizoidhinishwa

Tozo za wakusanyaji na watawanyaji wa mizigo zilizoidhinishwa zitakuwa ni zifuatazo:
(a)tozo ya kukabidhi mzigo;
(b)tozo ya utawanyaji wa mzigo;
(c)tozo ya kuhudumia vyombo vya moto;
(d)tozo ya ukusanyaji wa mzigo;
(e)tozo ya utafutaji wa mzigo; na
(f)tozo nyinginezo kama zitakavyoelekezwa katika amri nyingine za kudhibiti.

5. Viwango vya juu vya tozo

Viwango vya juu vya tozo zilizoidhinishwa za ukusanyaji na utawanyaji wa mzigo vitakuwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Amri hii.

Sehemu ya tatu – Masharti ya jumla

6. Urejeshaji wa gharama

Mkusanyaji na mtawanyaji wa mizigo anaweza kudai kurejeshewa na mpokeaji wa mzigo gharama zilizolipwa kwa wakala wa meli au mwendeshaji wa bandari au bandari kavu kwa kugawanya gharama hizo kwa uwiano wa ukubwa wa mzigo wa kila mpokeaji wa mzigo kama ilivyooneshwa katika hati ya mzigo majini.

7. Uzingatiaji maelekezo ya kudhibiti

Wakusanyaji na watawanyaji wa mizigo watapaswa kuzingatia yafuatayo:
(a)kutunza vitabu vya hesabu na kuhakikisha vinakaguliwa kwa wakati;
(b)kutoa ankara kwa wapokeajia wa mzigo zinazoonesha, pamoja na mambo mengine, idadi ya wapokeaji wa mzigo na ukubwa wa jumla wa mzigo uliokuwa katika hati ya mzigo majini;
(c)kubandika katika sehemu ya wazi viwango vya tozo zinazotumika, ambavyo havizidi viwango vya juu vilivyoidhinishwa, kwa ajili ya wateja kuona;
(d)kuwaruhusu wateja kuona au kuthibitisha gharama zinazorejeshwa kutokana na malipo yaliyofanywa kwa wakala wa meli, mwendeshaji wa bandari au bandari kavu;
(e)kuambatisha katika ankara za wateja nakala ya risiti za malipo yaliyofanywa kwa wakala wa meli, mwendeshaji wa bandari au bandari kavu; na
(f)kuhakikisha gharama zozote za wakusanyaji wa mzigo walio katika bandari za nje ya nchi hazilipwi na wapokeaji wa mizigo nchini;

8. Uunganishaji wa mifumo

Mkusanyaji na mtawanyaji wa mizigo atapaswa kufanya yafuatayo:
(a)kutumia mifumo sahihi ya TEHAMA kuwezesha utoaji wa hati za kielekroniki za makabidhiano ya mizigo ili kulinda mzigo katika hatua za makabidhiano; na
(b)kuunganisha mfumo wake wa TEHAMA na mfumo wa pamoja wa TEHAMA na inapolazimu kuunganisha mfumo wake na mifumo ya bandari nabandari kavu ili kuwezesha utumaji kielektroniki wa hati za kukabidhi mzigo.

9. Kuisha kwa muda wa Hati ya Kukabidhi Mzigo

Shirika litatangaza muda wa chini wa kuisha matumizi kwa Hati ya Kukabidhi Mzigo iliyotolewa na mkusanyaji na mtawanyaji wa mzigo kwa mpokeaji wa mzigo ili kuongeza ufanisi na kulinda mzigo katika hatua za ugomboaji.

10. Ufutaji wa Amri

Amri ya Tozo Na SMTRA/02/2018 kuhusu Tozo za Wakusanyaji na Watawanyaji wa Mzigo inafutwa.[SMTRA/02/2018]

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 5)

Iwango vya juu vya tozo vilivyoidhinisvhwa

TozoInatozwa kwaKiwango cha juu
Tozo ya kukabidhi mzigoHati ndogo ya mzigo majiniDola za Kimarekani 5 (bila Kodi ya Ongezeko la Thamani)
Tozo ya utawanyaji mzigoHati ndogo ya mzigo majiniDola za Kimarekani 100 (bila Kodi ya Ongezeko la Thamani)
Tozo ya kuhudumia vyombo vya motoHati ndogo ya mzigo majiniDola za Kimarekani 30 (bila Kodi ya Ongezeko la Thamani)
Tozo ya ukusanyaji mzigoHati ndogo ya mzigo majiniDola za Kimarekani 100 (bila Kodi ya Ongezeko la Thamani)
Tozo ya utafutaji mzigoTaniDola za Kimarekani 5 (bila Kodi ya Ongezeko la Thamani)
▲ To the top

History of this document

14 April 2023
Commenced
13 March 2023
Assented to