Kanuni za Ufanyaji Kazi Bila Kutumia Zana za Mwaka 2023

Government Notice 290 of 2023

Kanuni za Ufanyaji Kazi Bila Kutumia Zana za Mwaka 2023

Tanzania
Factories Act

Kanuni za Ufanyaji Kazi Bila Kutumia Zana za Mwaka 2023

Tangazo la Serikali 290 ya 2023

[Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 109]

1. Jina

Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Ufanyaji Kazi Bila Kutumia Zana za Mwaka 2023.

2. Tafsiri

Katika Kanuni hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—"hatari"maana yake ni uwezekano wa kupata jeraha, maumivu au ugonjwa kutokana na kukumbwa na kihatarishi;"kihatarishi" maana yake ni uwezekano wa kusababisha jeraha, maumivu au ugonjwa;"kitu" inajumuisha kitu kisicho hai au chenye uhai, mtambo na kitu chochote au viambata vilivyomo ndani ya kitu;"matatizo ya misuli na mifupa" maana yake ni jeraha, maumivu au ugonjwa unaotokea kwa ujumla au kwa sehemu kutokana na ufanyaji kazi bila kutumia zana mahali pa kazi, uwe unatokea ghafla au kwa muda mrefu, lakini haijumuishi jeraha, maumivu au ugonjwa unaosababishwa na kupondwa, kunaswa au kukatwa kunakotokana na uendeshaji wa mitambo;"matumizi ya nguvu kubwa" kuhusiana na ufanyaji kazi bila kutumia zana, maana yake ni matumizi ya nguvu ambayo ingetarajiwa kwamba watu wengi mahali pa kazi, au watu wanaoweza kufanya kazi hiyo, watakuwa na ugumu katika kuitekeleza na inajumuisha nguvu inayohitajika kunyanyua vitu vizito, kusukuma au kuvuta vitu ambavyo ni vigumu kusogeza, kuendesha zana zilizoundwa kwa mkono mmoja ikiwa ni lazima kwa mikono miwili kutumika, na kutumia zana zinazohitaji kubana kwa vishikizo vilivyo na umbali kati yao;Sheria” maana yake ni Sheria ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi; na"ufanyaji kazi bila kutumia zana" maana yake ni kazi yoyote anayoifanya mfanyakazi inayohitaji matumizi ya nguvu kuinua, kusukuma, kuvuta, kubeba, kusogeza, kushikilia au kuzuia kitu chochote.[Sura ya 297]

3. Matumizi

Kanuni hizi zitatumika katika maeneo yote ya kazi ambayo yanahusisha ufanyaji kazi bila kutumia zana.

4. Wajibu wa mtu zaidi ya mmoja

Pale ambapo, kwa mujibu wa Kanuni hizi, wajibu umewekwa kwa mtu zaidi ya mmoja, wajibu huo lazima ufanywe na kila mtu kwa masuala ambayo mtu huyo ana usimamizi au udhibiti nayo na kama mtu mwingine yeyote anawajibika au la kwa ajili ya kutekeleza wajibu huo.

5. Utambuzi na tathmini ya hatari za kazi zinazohusisha ufanyaji kazi bila kutumia zana

5. Pale ambapo mwajiri, chini ya kanuni ya 10 na 11 anahitajika kufanya utambuzi au tathmini ya hatari za kazi zinazohusisha ufanyaji kazi hatarishi bila kutumia zana, mwajiri anaweza kufanya utambuzi au tathmini ya hatari kwa aina za kazi kuliko utambuzi na tathmini ya hatari kwa kazi za mfanyakazi mmoja mmoja ikiwa —
(a)kazi zote za aina hiyo zinafanana; na
(b)utambuzi au tathmini ya hatari iliyofanywa kwa aina za kazi haisababishi mtu yeyote kuwekwa kwenye hatari tofauti kama tathmini ya hatari ingefanywa kwa kila kazi ya mtu mmoja mmoja.

6. Wajibu wa wasanifu, watengenezaji, waagizaji na wasambazaji

(1)Mtu ambaye anasanifu, anatengeneza, anaingiza au anasambaza mtambo wowote kwa ajili ya matumizi mahali pa kazi atahakikisha kwamba hatari yoyote ya matatizo ya misuli na mifupa ambayo inaweza kutokea wakati mtambo unatumiwa ipasavyo mahali pa kazi—
(a)imeondolewa; au
(b)ikiwa haiwezekani kuondoa hatari, itapunguzwa kadri inavyowezekana.
(2)Kwa madhumuni ya kanuni hii, mtambo wowote haupaswi kuchukuliwa kama unatumika ipasavyo pale unapotumika bila kuzingatia taarifa muhimu au ushauri wowote unaopatikana kuhusiana na matumizi yake.

7. Tathmini ya hatari

(1)Mwajiri ambaye amezingatia masharti ya tathmini ya hatari chini ya kifungu cha 60 cha Sheria, atazingatia pia kanuni ya 10 na 11 ya Kanuni hizi kuhusiana na kazi inayohusisha ufanyaji kazi hatarishi bila zana, endapo tathmini hiyo imezingatia hatari ya matatizo ya misuli na mifupa inayoweza kumuathiri mfanyakazi kutokana na kazi hiyo.
(2)Mwajiri atatakiwa kuzingatia masharti ya udhibiti wa hatari chini ya kanuni ya 11 ya Kanuni hizi, na iwapo hatua za kudhibiti hatari zilizopo zinadhibiti hatari ya matatizo ya misuli na mifupa inayoweza kumuathiri mfanyakazi.
(3)Pale ambapo kanuni ndogo ya (1) inatumika, mwajiri atazingatia wajibu chini ya kanuni ya 10 na kuweka kumbukumbu ya tathmini ya hatari iliyofanyika.
(4)Kanuni hii haizuii wajibu wa mwajiri kuchukua hatua za ziada za udhibiti wa hatari ya matatizo ya misuli na mifupa inayoweza kumuathiri mwajiriwa, ikiwa tathmini ya hatari au hatua za udhibiti wa hatari zilizochukuliwa hazitoshelezi.

8. Wajibu wa mwajiri kwa mkandarasi anayejitegemea na Majukumu mengine yanayohusiana

Kwa madhumuni ya kanuni hii—
(a)"mfanyakazi" inamjumuisha mkandarasi wa kujitegemea aliyepewa kazi na mwajiri na wafanyakazi wote wa mkandarasi anayejitegemea; na
(b)wajibu wa mwajiri chini ya kanuni hii umeongezwa kwa mkandarasi huyo anayejitegemea na mwajiriwa wa mkandarasi anayejitegemea, kuhusiana na masuala ambayo mwajiri—
(i)ana udhibiti; au
(ii)angekuwa na udhibiti lakini kwa makubaliano yoyote kati ya mwajiri na mkandarasi anayejitegemea ana udhibiti bila kujali makubaliano.

9. Mwajiri kushauriana na mwakilishi wa afya na usalama

Mwajiri anapotekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Kanuni hizi atatakiwa kushauriana na wawakilishi wa afya na usalama kuhusu utambuzi, tathmini au udhibiti wa hatari za ufanyaji kazi bila kutumia zana kulingana na mazingira yatakavyokuwa.

10. Wajibu wa mwajiri wa kutambua kazi hatarishi zinazohusisha ufanyaji kazi bila kutumia zana

(1)Mwajiri atahakikisha kwamba kazi yoyote inayofanywa, au itakayofanywa na mfanyakazi inayohusisha ufanyaji kazi hatarishi bila kutumia zana inatambuliwa.
(2)Katika Kanuni hizi “ufanyaji kazi hatarishi bila kutumia zana" unajumuisha—
(a)ufanyaji kazi bila kutumia zana wenye sifa zozote zifuatazo—
(i)matumizi ya nguvu ya kujirudia rudia au endelevu;
(ii)mkao mbaya wa kujirudia rudia au endelevu;
(iii)usogeaji unaojirudia rudia au endelevu;
(iv)matumizi ya nguvu kubwa; na
(v)kukumbwa na mitetemo endelevu.
(b)kunyanyua, kubeba au kusogeza watu au wanyama hai;
(c)kunyanyua, kubeba au kusogeza mizigo isiyo imara au isiyo na usawa au mizigo ambayo ni vigumu kushikika.
(3)Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), mwajiri atahakikisha kuwa kazi yoyote inayohusisha ufanyaji kazi hatarishi bila kutumia zana inatambuliwa—
(a)kabla ya kazi yoyote inayohusisha ufanyaji kazi bila zana inafanywa kwa mara ya kwanza mahali pa kazi;
(b)kabla marekebisho yoyote hayajafanyika kwa vitu vinavyotumika mahali pa kazi au mifumo ya kazi pamoja na kazi inayohusisha ufanyaji kazi bila zana, ikijumuisha mabadiliko ya mahali ambapo kazi hiyo inafanyika;
(c)kabla ya kitu kutumika kwa madhumuni mengine tofauti na ambayo kiliundwa ikiwa madhumuni mengine yanaweza kusababisha hatari ya ufanyaji kazi bila zana;
(d)ikiwa maelezo mapya au ya ziada kuhusu ufanyaji kazi hatarishi bila zana yanayohusishwa na kazi yamemfikia mwajiri; na
(e)ikiwa kuna taarifa imetolewa na au kwa niaba ya mfanyakazi ya uwepo wa tatizo la misuli na mifupa mahali pa kazi.

11. Wajibu wa mwajiri kufanya tathmini ya hatari

(1)Endapo kazi inayohusisha ufanyaji kazi hatarishi bila kutumia zana umetambuliwa kwa mujibu wa kanuni ya 10, mwajiri atahakikisha kwamba tathmini inafanywa ili kubaini kama kuna hatari yoyote ya matatizo ya misuli na mifupa inayotokana na kazi hiyo.
(2)Mwajiri atahakikisha kwamba tathmini inazingatia mambo yafuatayo yanayohusiana na utekelezaji wa kazi inayotathminiwa—
(a)mikao iliyokubaliwa;
(b)usogeaji unaotumika;
(c)kiasi au kiwango cha nguvu zinazotumika;
(d)hali ya mazingira, inayojumuisha joto, baridi na mitetemo, ambayo humkumba moja kwa moja mtu anayefanya kazi; na
(e)muda wa ufanyaji kazi na muda wa urudiaji kazi.
(3)Mwajiri atahakikisha kwamba tathmini ya hatari inapitiwa upya na, inapobidi, inarekebishwa, au tathmini nyingine ya hatari inafanywa ikiwa, kutokana na hali yoyote iliyotajwa katika kanuni ndogo ya 2(b) hadi (e) au kwa sababu nyingine yoyote, tathmini ya hatari iliyotajwa kwanza haitathmini vya kutosha hatari ya matatizo ya misuli na mifupa yanayomuathiri mfanyakazi kutokana na kazi husika.
(4)ambapo tathmini ya hatari iliyofanywa kwa mujibu wa kanuni hii itabainisha kuwa kuna hatari ya matatizo ya misuli na mifupa inayomuathiri mfanyakazi, mwajiri atahakikisha kwamba mbinu zilizotumiwa kutathmini hatari na matokeo ya tathmini yanarekodiwa na kutunzwa hadi tathmini mpya ya hatari itakapohitajika kufanyika kwa mujibu wa kanuni hii au ikiwa kazi husika haitafanyika tena.

12. Wajibu wa mwajiri kudhibiti hatari

(1)Mwajiri atahakikisha kwamba hatari yoyote ya matatizo ya misuli na mifupa inayoathiri mfanyakazi—
(a)imeondolewa; au
(b)ikiwa haiwezekani kuondoa au kupunguza hatari, vitu au utaratibu wa kazi utabadilishwa na mwajiri atahakikisha kuwepo kwa njia salama za ufanyaji kazi.
(2)Mwajiri haruhusiwi kutumia taarifa, mafunzo au maelekezo ya mbinu ya ufanyaji kazi bila kutumia zana kama njia pekee au msingi wa kudhibiti hatari isipokuwa kama njia zifuatazo za kudhibiti hatari hazitekelezeki—
(a)kuboresha—
(i)mahali pa kazi, au hali ya mazingira, ikijumuisha joto, baridi na mtetemo, ambapo kazi inayohusisha ufanyaji kazi bila kutumia zana hufanyika; au
(ii)mifumo ya kazi inayotumika kutekeleza kazi inayohusisha ufanyaji kazi bila kutumia zana;
(b)kubadilisha vitu vinavyotumika katika ufanyaji kazi bila kutumia Zana; au
(c)kutumia zana saidizi.

13. Wajibu wa mfanyakazi

Mfanyakazi atashirikiana na mwajiri kuhusiana na hatua yoyote iliyochukuliwa kwa madhumuni ya kuzingatia sharti lolote lililowekwa kwa mwajiri katika kanuni za 10, 11 na 12.
▲ To the top

History of this document

07 April 2023 this version