Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isakalilo ya mwaka 2023

Government Notice 300 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isakalilo ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isakalilo ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 300 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isakalilo ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mipangokina ya eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Jedwali (limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—"Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P1 yenye majira - nukta 791917MS, 9138107KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 1.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P2 yenye majiranukta 792452MS, 9136967KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P3 yenye majiranukta 792750MS, 9136528KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Mashariki kwa umbali wa kilomita 2.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P4 yenye majiranukta 787698MS, 9132627KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 2.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P5 yenye majira - nukta 785994MS, 9134462KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 1.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P6 yenye majira - nukta 786505MS, 9135995KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 3.0 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P7 yenye majira - nukta 788959MS, 9135676KZ; baada ya hapo unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 1.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P8 yenyemajira -nukta 789701MS, 9136518KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 2.1 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P9 yenye majira - nukta 791366MS, 9137379KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini-Mashariki kwa umbali wa kilomita0.9 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

07 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to