Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isimani ya mwaka 2023

Government Notice 301 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isimani ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isimani ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 301 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Isimani ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mipangokina ya eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Jedwali (limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P1 yenye majira - nukta 808952MS, 9175123KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.5 hadi barabara kuu ya Dodoma ukielekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 3.0 kwa kufuata mpaka wa kijiji cha Isimani hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P2 yenye majira - nukta 811839MS, 9173092KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 1.45 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P3 yenye majira - nukta 811151MS, 9171797KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi kwa umbali wa kilomita 2.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P4 yenye majira - nukta 809030MS, 9172569KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi kwa umbali wa kilomita 0.63 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P5 yenye majira - nukta 808430MS, 9172783KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 2.4 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

07 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to