Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Idodi ya mwaka 2023

Government Notice 308 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Idodi ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Idodi ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 308 ya 2023

  • Imechapishwa katika Gazette of the United Republic of Tanzania 15 hadi 28 Aprili 2023
  • Imeidhinishwa tarehe 17 Machi 2023
  • Ilianza tarehe 28 Aprili 2023
  • [Hili ni toleo la hati hii kutoka 28 Aprili 2023.]
  • [Kumbuka: Hati asili ya uchapishaji haipatikani na maudhui haya hayakuweza kuthibitishwa.]
(Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1))

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Idodi ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mipangokina ya eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Jedwali (limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P1 yenye majira - nukta 745328MS, 9141203KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 0.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P2 yenye majira nukta 744778MS, 9140859KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 1.8 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P3 yenye majira - nukta 743307MS, 9139689KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 1.28 hadi mto Idodi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P4 yenye majira - nukta 742413MS, 9138771KZ; baada ya hapo mpaka unaeleka Kusini kwa umbali wa kilomita 3.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P5 yenye majira - nukta 739307, 9137816; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa kufuata korongo la mto hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P6 yenye majira - nukta 738947, 9139109; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 1.5 kwa kulifuata korongo la mto Idodi hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P7 yenye majira - nukta 740163, 9140035; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazin - Mashariki kwa umbali wa kilomita 1.1 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P8 yenye majira - nukta 741125, 9140621; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 2.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P9 yenye majira - nukta 743334, 914144; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 1.1 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P10 yenye majira - nukta 744238, 9142186; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilometa 0.8 hadi barabara ya Iringa - Ruaha National Park kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P11 yenye majira - nukta 744900, 9141689; hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
Published in Gazette of the United Republic of Tanzania 15
Commenced
17 March 2023
Assented to