Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ibolelo - Mwabasabi ya mwaka 2023

Government Notice 309 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ibolelo - Mwabasabi ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ibolelo - Mwabasabi ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 309 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ibolelo - Mwabasabi ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpangokina wa eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 419107.32MS, 9679622.87KZ; baada ya hapo mpaka unalekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ79°38'41"MG kwa umbali wa kilometa 1.3 kuelekea barabara ya Mwatulole kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 417899.63MS, 9680172.28KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS156°45'05"MG hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 417135.58MS, 9680188.46KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS150°56'35"MG kwa umbali wa kilomita 0.53 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 416665.52MS, 9679940.07KZ; baada ya hapo mpaka unafuata barabara ya Mwatulole kuelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS156°09'27"MG kwa umbali wa kilometa 0.43 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira - nukta 416395.21MS, 9679598.07KZ; baada ya hapo mpaka unafuata bonde kuelekea Kusini - Mahariki katika uelekeo wa KS98°06'49"MS kwa umbali wa kilometa 1.56 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira - nukta 417476.10MS, 9678461.93KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS156°04'17"MS kwa umbali wa kilomita 0.69 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba G yenye majira - nukta 418115.69MS, 9678197.02KZ; baada ya hapo mpaka unafuata bonde la mto kuelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KS102°19'06"MG kwa umbali wa kilomita 1.7 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to