Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Kakubilo Kikwete Centre ya mwaka 2023

Government Notice 310 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Kakubilo Kikwete Centre ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Kakubilo Kikwete Centre ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 310 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Kakubilo Kikwete Centre ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Utangazaji wa eneo la upangaji

Mpangokina wa eneo Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 397672MS, 9714009KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS155°MG kwa umbali wa kilomita 4.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 396667MS, 9713536KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi kwa kukatiza barabara mbili katika uelekeo wa MG48° kwa umbali wa kilomita 3.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 393296MS, 9713553KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS143°MS kwa umbali wa kilomita 4.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 395961MS, 9710543KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa KS130° kwa umbali wa kilomita 1.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira - nukta 396074MS, 9709045KZ; baada ya hapo mpaka unaeleka Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS78°MS kwa umbali wa kilomita 1.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira - nukta 397468MS, 9708039KZ; baada ya hapo mpaka unaeleka Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KZ143°MS kwa umbali wa kilomita 2.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba G yenye majira - nukta 398509MS, 9710437KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ78°MG kwa umbali wa kilomita 3.6 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to