Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ikina - Bukoli ya mwaka 2023

Government Notice 314 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ikina - Bukoli ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ikina - Bukoli ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 314 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Ikina - Bukoli ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpangokina wa eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 425883MS, 9644235KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa KZ107° kwa umbali wa kilomita 3.78 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 426184MS, 9647999KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ77°MG kwa umbali wa kilomita 3.82 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 426184MS, 9647999KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa KS164° kwa umbali wa kilomita 2.09 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 422313MS, 9647345KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS123°MS kwa umbali wa kilomita 1.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira - nukta 422537MS, 9645644KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS170°MS kwa umbali wa kilomita 2.56 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira - nukta 428440MS, 9644530KZ; baada ya hapo mpaka unakatiza barabara ukielekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa MS79°KS hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to