Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Nzera Centre ya mwaka 2023

Government Notice 316 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Nzera Centre ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Nzera Centre ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 316 ya 2023

  • Imechapishwa katika Gazette of the United Republic of Tanzania 15 hadi 28 Aprili 2023
  • Imeidhinishwa tarehe 17 Machi 2023
  • Ilianza tarehe 28 Aprili 2023
  • [Hili ni toleo la hati hii kutoka 28 Aprili 2023.]
  • [Kumbuka: Hati asili ya uchapishaji haipatikani na maudhui haya hayakuweza kuthibitishwa.]
[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Nzera Centre ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpangokina wa eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—"Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 401578MS, 9713273KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa MS161° kwa umbali wa kilomita 1.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 405930MS, 9713273KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KZ52°MS kwa umbali wa kilomita 0.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 409186MS, 9714307KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ204°MG kwa umbali wa kilomita 0.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 405410MS, 9716863KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ57°MG kwa umbali wa kilomita 0.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira - nukta 402961MS, 9720803KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS120°MG kwa umbali wa kilomita 0.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira - nukta 400295MS, 9715126KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS125°MS kwa umbali wa kilomita kilomita 0.2 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
Published in Gazette of the United Republic of Tanzania 15
Commenced
17 March 2023
Assented to