Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Lwamgasa ya mwaka 2023

Government Notice 317 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Lwamgasa ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Lwamgasa ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 317 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Lwamgasa ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpango kina wa eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Jedwali [Limetengenezwa chini ya aya ya 2]

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 388202MS, 9646632KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS137°MS kwa umbali wa kilomita 4.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 388109MS, 9652706KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KZ152°MS kwa umbali wa kilomita 2.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 396829MS, 9660911KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika ueleko wa KZ105°MS kwa umbali wa kilomita 4.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 396824MS, 9652604KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ138°MG kwa umbali wa kilomita 2.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira - nukta 395137MS, 9659425KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa KZ142° kwa umbali wa kilomita 3.9 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira - nukta 396834MS, 9660932KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ82°MS kwa umbali wa kilomita 0.8 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba G yenye majira - nukta 397701MS, 9659613KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS156°MG kwa umbali wa kilomita 1.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba H yenye majira - nukta 397381MS, 9655621KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa MG142° kwa umbali wa kilomita 3.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba I yenye majira - nukta 399694MS, 9652649KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa MG135° kwa umbali wa kilomita 3.8 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba J yenye majira - nukta 395054MS, 9646489KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS154°MS kwa umbali wa kilomita 3.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba K yenye majira - nukta 3926426MS, 9645219KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS95°MG kwa umbali wa kilomita 2.7 hadi ulipoanzia.”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to