Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Tungamalenga ya mwaka 2023

Government Notice 318 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Tungamalenga ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Tungamalenga ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 318 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Tungamalenga ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mipangokina wa eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alamaya mpaka ya upimaji namba P1 yenye majira - nukta 732662MS, 9134512KZ kwa umbali wa kilomita 1.0 kutoka barabara ya Iringa-Ruaha National Park baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilometa 1.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P2 yenye majira - nukta 731835MS, 9133331KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa kufuata korongo kwa umbali wa kilomita 0.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P3 yenye majira - nukta 731835MS, 9132752KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 0.65 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P4 yenye majira - nukta 731898MS, 9132101KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Magharibi kwa umbali wa kilomita 0.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P5 yenye majira - nukta 731605MS, 9131910KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P6 yenye majira - nukta 731224MS, 9131847KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 1.7 kwa kufuata korongo hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P7 yenye majira - nukta 730406MS, 9133117KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini-Magharibi kwa umbali wa kilomita 0.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P8 yenye majira - nukta 730025MS, 9132974KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa kufuata korongo la mto Tungamalenga hadi kwenye barabara ya Iringa-Ruaha National park kwa umbali wa kilomita 0.8 hadi kwenye alama ya upimaji ya mpaka ya upimaji namba P9 yenye majira - nukta 729835MS, 9133781KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa kufuata mto Tungamalenga kwa umbali wa kilomita 1.1hadi kwenye alama ya ya mpaka ya upimaji namba P10 yenye majira - nukta 731332MS, 9136178KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.4 hadi kwenya alama ya mpaka ya upimaji namba P11 yenye majira - nukta 731702MS, 9136252KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 1.1 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P12 yenye majira - nukta 731971MS, 9135147KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 0.9 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to