Amri ya Kupanga Eneo la Kompaund ya Mwaka 2023

Government Notice 320 of 2023

Amri ya Kupanga Eneo la Kompaund ya Mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kupanga Eneo la Kompaund ya Mwaka 2023

Tangazo la Serikali 320 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kupanga Eneo la Kompaund ya Mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la pangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[sura ya 355]

3. Mpango wa jumla na kina wa eneo

Mipango ya jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Geita.

Jedwali (limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A kwenye barabara ya kuelekea GGM yenye majira-nukta 412839MS, 9681712KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa 84o kwa umbali wa kilometa 0.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 412656MS, 9682283KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa 87o kwa umbali wa kilometa 0.26 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 412411MS, 9682189KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa 72o kwa umbali wa kilometa 0.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 412398MS, 9682393KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa 154o kwa umbali wa kilometa 0.45 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira-nukta 412180MS, 9682781KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa 73o kwa umbali wa kilometa 0.97 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majiranukta 411508MS, 9682079KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa 98o kwa umbali wa kilometa 0.43 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba ‘G’ yenye majira - nukta 411049MS, 969681.651KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa 157o kwa umbali wa kilometa 0.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba H yenye majira - nukta 411051MS, 9682079KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa 137o kwa umbali wa kilomita 1.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba I yenye majiranukta 412568MS, 9681656KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeowa 93o kwa umbali wa kilometa 0.4 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to