Amri ya Kupanga Eneo la Mgusu ya Mwaka 2023

Government Notice 321 of 2023

Amri ya Kupanga Eneo la Mgusu ya Mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kupanga Eneo la Mgusu ya Mwaka 2023

Government Notice 321 of 2023

(Imetengenezwa Chini ya Kifungu cha 8(1))

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kupanga Eneo la Mgusu ya Mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpango wa jumla na kina wa eneo

Mipango ya Jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 394603MS, 9684845KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa 1490 kwa umbali wa kilometa 2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira-nukta 395932MS, 9683352KZ; baada ya hapo mpaka unafuata mpaka wa hifadhi ya msitu wa Geita upande wa Mashariki katika uelekeo wa 1060 kwa umbali wa kilometa0.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji nambaE yenye majira - nukta 396388MS, 9683572KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa 1100 kwa umbali wa kilometa 1.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira-nukta 396213MS, 9685272KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa 1240 kwa umbali wa kilometa 0.24hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majiranukta 395119MS, 9685861KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa 1040 kwa umbali wa kilometa 0.87 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 394533MS, 9685215KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa 1270 ukikutana na barabara ya Mgusu kwa umbali wa kilometa 0.37 hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to