Amri ya Kupanga Eneo la Nshinde ya Mwaka 2023

Government Notice 325 of 2023

Amri ya Kupanga Eneo la Nshinde ya Mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kupanga Eneo la Nshinde ya Mwaka 2023

Government Notice 325 of 2023

(Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1))

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kupanga Eneo la Nshinde ya Mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpango wa jumla na kina wa eneo

Mipango ya jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenyemajira-nukta 420898MS, 9679277KZ; baada ya hapo mpaka unaelekeaKaskazini katika uelekeo wa 570kwa umbali wa kilometa 1.48 kupitia barabara ya Mwatulole - Magogo hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 419510MS, 9679812KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa 1050 kwa umbali wa kilometa 1.62 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 418556MS, 9678500KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Masharikikatika uelekeo wa 870 kwaumbali wa kilometa 0.81 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira-nukta 419238MS, 9678053KZ’ hadi ulipoanzia”
▲ To the top

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to