Notisi ya Uteuzi wa Mwendesha Mashitaka ya mwaka 2023

Government Notice 40 of 2023

Notisi ya Uteuzi wa Mwendesha Mashitaka ya mwaka 2023

Tanzania
National Prosecutions Service Act, 2008

Notisi ya Uteuzi wa Mwendesha Mashitaka ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 40 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 22]

1. Jina

Notisi hii itaitwa Notisi ya Uteuzi wa Mwendesha Mashitaka ya mwaka 2023.

2. Uteuzi wa waendesha mashitaka

Mtu ambaye jina lake limetajwa kwenye Jedwali la Notisi hii ameteuliwa kuwa mwendesha mashitaka kwa madhumuni ya kuendesha mashauri ya jinai kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa masuala yaliyoainishwa kwenye Sheria ya Usajili wa Wasanifu na Wapima Majengo.[Sura ya 269]

3. Uhalali wauteuzi

(1)Uteuzi uliofanywa chini ya Notisi hii utakuwa halali kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Notisi hii.
(2)Bila kujali aya ndogo ya (1), mtu aliyeteuliwa kama mwendesha mashtaka anaweza kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi kinachopungua miaka mitano endapo ajira ya mtu huyo kwenye Utumishi wa Umma itakoma au endapo uteuzi wa mtu huyo utaamuliwa vinginevyo na Mkurugenzi wa Mashtaka.

Jedwali

Uteuzi wa mwendesha mashitaka

Na.Jina
1.Ibrahim Mohamed
▲ To the top

History of this document

10 February 2023 this version
02 February 2023
Assented to