Tanzania
Magistrates’ Courts Act
Amri ya Kubadilisha Mamlaka ya Mahakama ya Wilaya Chato ya mwaka 2023
Tangazo la Serikali 92 ya 2023
- Imechapishwa katika Gazette of the United Republic of Tanzania 6 hadi 17 Februari 2023
- Imeidhinishwa tarehe 8 Februari 2023
- Ilianza tarehe 17 Februari 2023
- [Hili ni toleo la hati hii kutoka 17 Februari 2023.]
1. Jina
Amri hii itajulikana kama Amri ya Kubadilisha Mamlaka ya Mahakama ya Wilaya Chato ya mwaka 2023.2. Mabadiliko ya mamlaka ya Mahakama ya Wilaya ya Chato
Mamlaka ya Mahakama ya Wilaya Chato yanayotolewa chini ya Sheria ya Mahakama za Mahakimu yanabadilishwa kama ilivyoanishwa katika Jedwali la Amri hii kwa madhumuni ya kusikilizana kuamua mashauri ya ainazote yaliyondani ya mamlaka ya awali, rufaa na mapitio ya mahakama ya wilaya.[Sura ya 11]3. Eneo la mamlaka
Mahakama ya Wilaya Chato, pamoja na mamlaka yake ndani ya Wilaya ya Chato, itakuwa na mamlaka katika eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii.History of this document
17 February 2023 this version
08 February 2023
Assented to