Kanuni za Uteuzi, Ujira na Nidhamu ya Wasuluhishi za mwaka 2024

Government Notice 827 of 2024


Tanzania
Judicature and Application of Laws Act

Kanuni za Uteuzi, Ujira na Nidhamu ya Wasuluhishi za mwaka 2024

Tangazo la Serikali 827 ya 2024

[Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 4]

Sehemu ya kwanza – Masharti ya utangulizi

1. Jina

Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Uteuzi, Ujira na Nidhamu ya Wasuluhishi za mwaka 2024.

2. Matumizi

Kanuni hizi zitatumika kwa wasuluhishi wanaofanya usuluhishi ulioamriwa na mahakama au walioteuliwa kwa ajili hiyo.

3. Tafsiri

Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—Jaji Mfawidhi” maana yake ni Jaji Mfawidhi wa Masjala ya Mahakama Kuu, Masjala ndogo au Divisheni;Kanuni za Maadili” maana yake ni Kanuni za Maadili na Mwenendo wa Wapatanishi, Wasuluhishi na Waamuzi;[TS. Na. 148 la 2021]ukiukaji wa maadili ya kitaaluma” maana yake ni kitendo chochote au kutotenda kunakochukuliwa kuwa ni ukiukaji wa Kanuni za Maadili; nausuluhishi ulioamriwa na mahakama” maana yake ni usuluhishi unaorejewa chini ya Amri ya Nane ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai.[Sura ya 33]

Sehemu ya pili – Uteuzi wa wasuluhishi

4. Matumizi ya Sehemu hii

Masharti ya Sehemu hii yatatumika kwa wasuluhishi ambao siyo maafisa wa mahakama wanaohudumu na waliostaafu.

5. Sifa za kuteuliwa kuwa msuluhishi

Mtu atastahili kuteuliwa kuwa msuluhishi chini ya Kanuni hizi iwapo mtu huyo ameidhinishwa kuwa mpatanishi, msuluhishi au mwamuzi chini ya Kanuni za Uidhinishaji wa Watoa Huduma za Upatanishi, Usuluhishi na Uamuzi.[TS. NA. 147 la 2021]

6. Utaratibu wa uteuzi

(1)Mtu anayekusudia kuteuliwa kuwa msuluhishi atawasilisha maombi ya uteuzi kwa Jaji Mkuu.
(2)Maombi chini ya kanuni hii yatakuwa katika Fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza na kuambatishwa na cheti cha uthibitisho kilichotolewa chini ya Kanuni za Uidhinishaji wa Watoa Huduma za Upatanishi, Usuluhishi na Uamuzi.[TS. Na. 147 ya 2021]

7. Uamuzi wa maombi

Baada ya kupokea maombi, Jaji Mkuu, ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kupokelewa kwa maombi hayo—
(a)ikiwa ameridhika kwamba mwombaji anastahili kuteuliwa, atakubali maombi na kumjulisha mwombaji kwa maandishi kuhusu kuteuliwa kwake; au
(b)kama hajaridhika na maombi—
(i)atamtaka mwombaji kutoa maelezo zaidi kwa ajili kuzingatiwa; au
(ii)atakataa maombi na kumjulisha mwombaj i kwa maandishi kuhusu kukataliwa huko na sababu zake.

8. Rejesta ya wasuluhishi

Msajili wa Mahakama Kuu atatunza rejesta ya wasuluhishi walioteuliwa chini ya Kanuni hizi.

Sehemu ya tatu – Ujira

9. Matumizi ya Sehemu hii sura ya 33

Masharti ya Sehemu hii yatatumika kwa wasuluhishi wote isipokuwa msuluhishi aliyechaguliwa na wadaawa chini ya kanuni ya 25(6)(f) ya Amri ya Nane ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai.

10. Ujira wa wasuluhishi

(1)Kwa kuzingatia masharti ya Sehemu hii, msuluhishi atastahili kulipwa ada ya huduma kwa kila shauri la upatanishi kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili.
(2)Bila ya kuathiri kanuni ndogo ya (1), pale ambapo ni muhimu kwa msuluhishi kusafiri, atastahili kupata posho za safari na kujikimu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili:Isipokuwa kwamba, pale ambapo msuluhishi ni afisa wa mahakama anayehudumu, gharama chini ya kanuni hii zitalipwa kwa mujibu wa masharti ya utumishi wake.

11. Wajibu wa kulipa wasuluhishi

Ujira, matumizi na gharama zinazopaswa kulipwa kwa msuluhishi chini ya Kanuni hizi zitalipwa na Mahakama.

Sehemu ya nne – Kanuni za maadilina hatua za kinidhamu

12. Matumizi na utekelezaji wa Kanuni za Maadili

(1)Kanuni za Maadili zitatumika pamoja na mabadiliko muhimu yanayofaa kwa wasuluhishi chini ya Kanuni hizi.
(2)Jaji Mfawidhi atatekeleza Kanuni za Maadili kwa madhumuni ya kudhibiti nidhamu ya wasuluhishi.
(3)Msuluhishi anayekiuka Kanuni za Maadili anakiuka maadili ya kitaaluma.

13. Adhabu kwa kukiuka kanuni za maadili

Msuluhishi anayekiuka maadili ya kitaaluma—
(a)ikiwa ni afisa wa mahakama anayehudumu, atawajibika kwa hatua za kinidhamu kama ilivyoainishwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mahakama; au
(b)katika hali nyingine yoyote, atawajibika kwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni hizi.
[Sura ya 237]

14. Malalamiko kuhusu ukuikwaji wa maadili ya kitaaluma

(1)Mtu ambaye hajaridhishwa na mwenendo wa msuluhishi na anaamini kuwa msuluhishi amekiuka maadili ya kitaaluma anaweza kuwasilisha malalamiko kwa Jaji Mfawidhi dhidi ya ukiukwaji huo.
(2)Malalamiko yatafanyika kwa maandishi katika lugha ya Kiingereza au Kiswahili yakiungwa mkono na nyaraka nyingine yoyote au taarifa kama uthibitisho wa malalamiko hayo.
(3)Kanuni hizi hazitatafsiriwa kumzuia Jaji Mfawidhi kuanzisha mashauri ya kinidhamu kwa utashi wake.

15. Uchunguzi wa malalamiko

(1)Jaji Mfawidhi, ndani ya siku saba baada ya kupokea malalamiko, ataamua kama malalamiko hayo ni ya msingi au ni uzushi na yasiyo na msingi.
(2)Endapo Jaji Mfawidhi ataridhika kwamba malalamiko ni ya msingi, kwa kuzingatia haki ya msuluhishi kusikilizwa, anaweza kutoa adhabu zifuatazo dhidi ya msuluhishi:
(a)kutoa onyo la maandishi;
(b)kumtaka kulipa kiasi cha fedha ambacho kinaweza kutosha kufidia gharama au hasara aliyopata mlalamikaji kutokana na malalamiko;
(c)kupendekeza kwa Jaji Mkuu kusimamishwa kazi au kutenguliwa kwa msuluhishi; au
(d)hatua nyingine yoyote kadri Jaji Mfawidhi atakavyoona inafaa.

Jedwali la kwanza (Limetengenezwa chiniya kanuniya 6(2))

Fomu MD

[Ujumbe wa uhariri: Fomu haijatolewa tena.]

Jedwali la pili (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10)

Ada na posho

Sehemu ya A: Ada ya huduma

 Maafisa wa mahakama wanaohudumu Wasuluhishi tofauti na maafisa wa mahakama wanaohudumu
Maelezo Ada
Kwa kila usuluhishi uliofanikiwa.Tshs. 500,000/= Tshs. 500,000/=
Kwa kila usuluhishi uliofanikiwa kwasehemu.Haitumiki Tshs. 300,000/=
Kwa kila usuluhishi usiofanikiwa.Haitumiki Tshs. 200,000/=

Sehemu ya B: Posho ya usafirina kujikimu

S/NAina ya usafiriDaraja
1AngaDaraja la Uchumi
2BahariDaraja la Kwanza
3TreniDaraja la Kwanza
4BarabaraDaraja la kifahari
5Ikiwa ni usafiri binafsiMsuluhishi atastahiki posho ya mafota kulingana na kiwango kinachotumiwa na Serikali
6Posho ya kujikimuIsiyozidi Tshs. 250,000/= kwa usiku
▲ To the top

History of this document

04 October 2024 this version
Commenced
26 September 2024
Assented to