Kanuni za Ada za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi za Mwaka, 2025

Government Notice 60 of 2025

Kanuni za Ada za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi za Mwaka, 2025

Tanzania
Employment and Labour Relations Act, 2004

Kanuni za Ada za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi za Mwaka, 2025

Tangazo la Serikali 60 ya 2025

[Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 98(2)(p)]

1. Jina

Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Ada za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi za Mwaka 2025.

2. Tafsiri

Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—Ada” maana yake ni malipo kwenda kwa Tume kwa ajili ya kupata huduma zilizoainishwa katika Jedwali la Kanuni hizi; naTume” maana yake ni Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Taasisi za Kazi.[Sura ya 300]

3. Adza na Tume

Ada zilizoainishwa katika Jedwali la Kanuni hizi zitalipwa kwa Tume kulingana na huduma zilizoainishwa kwenye Jedwali hilo.

4. Msamaha wa kutokulipa ada

(1)Serikali haitawajibika kulipa ada kuhusiana na shauri lolote itakalofungua au litakalofunguliwa dhidi yake mbele ya Tume.
(2)Endapo mkataba wowote ulioingiwa na Jamhuri ya Muungano na nchi nyingine yoyote unaeleza kwamba ada hazitalipwa kwa ajili ya shauri lolote, ada zilizoainishwa katika Jedwali hazitalipwa kuhusiana na shauri husika.[Sura ya 21]
(2)Mtu ambaye amepewa msaada wa kisheria chini ya Sheria ya Msaada wa Kisheria kuhusiana na shauri aliloanzisha au lililoanzishwa dhidi yake hatalipa ada anazopaswa kulipa kwa Tume chini ya Kanuni hizi.[Tafadhali kumbuka: Nambari kama ilivyo kwenye asili.]
(3)Mkurugenzi Mkuu anaweza, iwapo atajiridhisha kwamba kuna mazingira maalum yanayomzuia mtu kulipa ada anayopaswa kulipa chini ya Kanuni hizi, kutoa msamaha kwa mtu huyo kutolipa ada husika.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 3)

Ada za huduma za Tume

Na.Huduma inayotolewaKiasi cha ada kwa kila huduma
1.Kusajili Fomu CMA F. 110,000/=
2.Kusajili Fomu CMA F. 1B10,000/=
3.Kuomba nakala ya mwenendo iliyothibitishwa (kwa kila ukurasa)100/=
4.Kupata nakala ya ziada ya tuzo au uamuzi mdogo (kwa kila ukurasa)200/=
5.Kusajili hati ya Makubaliano20,000/=
6.Kuwasilisha nyaraka nyingine yoyote ambayo haijabainishwa katika Jedwali hili2,000/=
7.Majibu ya maombi mengine yoyote2,000/=
8.Maombi ya kupitia jalada la shauri5,000/=
9.Kuwasilisha maombi chini ya Hati ya dharura100,000/=
10.Maombi ya kuongeza muda wa kusajili nyaraka nje ya muda20,000/=
11.Kusajili shauri la madai ya gharama30,000/=
12.Kuwasilisha Taarifa ya Pingamizi na Kiapo Kinzani20,000/=
13.Kurekebisha Nyaraka za Maombi10,000/=
14.Maombi mengine yoyote10,000/=
15.Maombi ya kuchelewa kusajili mgogoro10,000/=
16.Maombi ya kutengua uamuzi wa upande mmoja20,000/=
17.Maombi ya kurejesha mgogoro20,000/=
18.Maombi ya kibali cha kukubaliwa kutoa huduma za msingi wakati wa mgomo au kufangia nje200,000/=
19.Maombi ya kutambua huduma kama huduma muhimu mbele ya Kamati ya Huduma Muhimu300,000/=
20.Kusajili mgogoro mbele ya Kamati ya Huduma Muhimu300,000/=
21.Ombi la kuteuliwa kwa huduma ya chini zaidi mbele ya Kamati ya Huduma Muhimu300,000/=
22.Maombi ya kuhamisha shauri20,000/=
23.Kusajili mgogoro wa haki za kiasasi100,000/=
24.Kusajili mgogoro wa kupunguza wafanyakazi100,000/=
25.Kusuluhisha mgogoro ambao haujawasilishwa rasmi mbele ya Tume100,000/=
▲ To the top

History of this document

31 January 2025 this version
21 January 2025
Assented to