TAARIFA KWA UMMA: UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA KIMAHAKAMA WAKATI HUU WA TAHADHARI YA JANGA LA COVID – 19 (KORONA) IMETOLEWA NA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA, JAJI MKUU WA TANZANIA, MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MWANZA, 23/03/2020

Attachment | Size |
---|---|
![]() | 549.68 KB |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA YA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA: UENDESHAJI WA
SHUGHULI ZA KIMAHAKAMA WAKATI HUU WA
TAHADHARI YA JANGA LA COVID - 19 (KORONA)
IMETOLEWA NA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA,
JAJI MKUU WA TANZANIA,
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MWANZA,
23/03/2020
Mahakama ya Tanzania ni Taasisi ya Umma inayotakiwa kutekeleza maelekezo na tahadhari mbali mbali ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Nawasihi watumishi wote wa Mahakama na wadau wetu
tufuatilie hizo taarifa ambazo ni muhimu kwetu pia.
Nimewaiteni kwa ajili ya kuwafahamisha kuhusu hatua mbali mbali ambazo tayari Mahakama ya Tanzania imechukua ili kuungana na jitihada za Serikali ambayo ndiyo yenye kauli ya mwisho kuhusu maswala ya afya na tahadhari mbali mbali.
Taarifa ya kina zaidi kuhusu nini hasa kinafanyika itatolewa na viongozi wa Mahakama waliopo Dar es Salaam hapo kesho.
Kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani alivyosema tarehe 18/3/2020-
*Don't assume your community won't be affected. Prepare us if it will be. [Mahakama na watumishi wote tujitayarishe, na tubainishe tumejitayarishaje kusaidia katika kuzuia kuenea. Na jumuiya ya Mahakama inagusa pia wafungwa, Mahabusu, Mawakili, wananchi walio na mashauri, na kadhalika.
*Don't assume you won't be infected. Prepare as if you will be [Tuwe na tahadhari, na tujitayarishe kwa lolote litakalotokea.
*But there is hope, there are many things all countered can do [Tunaweza kusaidia kwa kupunguza msongamano na kuchangia kuzuia kusambaa. [Wadau wetu ni lazima wakubali masharti ambayo tumeweka. Kwa mfano, hakuna wasindikizaji, kunawa mikono, kutumia mitandao zaidi].
*Virus is presenting us with unprecedented threat, but it is also gives us the opportunity to adjust our lives and the way we deliver justice.
Kuna hatua kadhaa ambazo Mahakama imechukua:
Kutumia TEHAMA zaidi na kuongeza maeneo ya matumizi ya TEHAMA.
Matumizi ya TEHAMA ni matunda ya mpango wa miaka mitano wa maboresho ya Mahakama. Haya maboresho yanatuwezesha kutumia zaidi TEHAMA katika kukabiliana na janga la Korona.
Moja ya hatua kubwa katika utekelezaji wa maboresho ambayo Mahakama imekuwa ikifanya ni matumizi ya Tehama katika kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama na kuzisogeza karibu na mwananchi.
Hii ni pamoja na matumizi ya mifumo ya Tehama katika usajili wa mashauri kielektroniki, usikilizaji wa mashauri kupitia Mahakama mtandao (video conferencing);
upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kimahakama kwa kupitia njia ya simu (SMS notification) na barua pepe pamoja na kupata taarifa na huduma mbali mbali kupitia tovuti ya Mahakama.
Mifumo hii yote inaruhusu mwananchi au mdaawa wa shauri kupata huduma hizi bila kumlazimu kufika katika Mahakama zetu hivyo kutoa fursa kwao kutumia muda huo katika shughuli za uzalishaji na utoaji huduma.
Mahakama imeweka mitambo ya kisasa ya TEHAMA kwenye:- Mahakama Kuu Masijala Kuu - DSM:- Mahakama Kuu Mbeya:- Mahakama Kuu Bukoba, Kituo cha Mafunzo Kisutu:- Chuo Cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto, Magereza ya Keko na Segerea.
Kwa hatua hii ambayo Mahakama imefikia TEHAMA ni njia na hatua mojawapo itakayowezesha Mahakama kukabiliana na maambukizi ya virusi vya COVID 19 hasa kupunguza na kuondoa mikusanyiko katika maeneo ya Mahakama.
Hadi hivi sasa Mahakama imeshachukua hatua mbalimbali na inaendelea kujipanga katika kukabiliana na janga hili.
Kwa mfano kwa kanda ya Dar es salaam ambapo mashauri ya jinai yalikwisha anza kusikilizwa kwa njia Mahakama Mtandao.
Kwa sasa mashauri yote ya jinai Jijini Dar es Salaam yanayoahirishwa kutokana na sababu mbalimbali, watuhumiwa waliopo katika gereza la Keko na Segerea, hawatalazimika kufikishwa Mahakamani, badala yake mashauri hayo yataahirishwa kwa njia ya Mahakama mtando ili kuepuka msongamano na mchanganyiko wa kuwaleta mahabusu na wafungwa Mahakamani.
Aidha kwa Kanda zenye vifaa vya Mahakama mtandao, utaratibu unakamilishwa wa uwekaji wa vifaa hivyo katika magereza yaliyopo katika Kanda hizo ili huduma kama hiyo pia iweze kutolewa, mfano Kanda ya Mbeya na Bukoba.
Juhudi za kuweka vifaa hivyo kwa kanda zingine zilizosalia zinaendelea na baada ya muda mfupi huduma kama hizo zitatolewa.
Kanuni za kufungua Mashauri kwa njia ya Mtandao (Electronic Filing Rules, 2018 GN 148/2018.
Hizi Kanuni zilianza kufanya kazi tangu tarehe 13/04/2018.
Hizi Kanuni ni muhimu sansa katika kufungua mashauri kimtandao na zitasambazwa ili wananchi na wadau watumie utaratibu wa kufungua mashauri mitandaoni bila kufika Mahakamani.
Kwa upande wa usajili wa mashauri kwa njia “E-FILING”. Mahakama inawasisitiza wadau wote kusajili mashauri kwa njia hii ya mitandao (online case registration) ili kupunguza msongamano na mchanganyiko wa watu ambao unaweza kueneza maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.
Mahakama inashauri wananchi, Mawakili wa Serikali na Mawakili wa kujitegemea kutoa ushirikiano hasa kwa upande wa mashauri ya madai kutumia njia hii ya kusajili mashauri online.
Hivi punde hata kesi za jinai zitasajiliwa na wahusika kupitia mitandao itakayotayarishwa kwa ajili hiyo.
Njia hii itasaidia sana si tu kupunguza maambukizi ya virus vya COVID 19, bali itawaondoshea adha ya usumbufu wa kusafiri kuja Mahakamani na pia muda huo utatumika kwa shughuli zingine za uzalishaji na za kijamii.
Wakati huu Mahakama inaendelea na kuchukua tahadhari kwa kupanua wigo wa matumizi ya Tehama ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa urahahisi bila kuwalazimu wadaawa na wananchi kufika Mahakamani.
Ni wito wa Mahakama kwa wadaawa na wananchi kutoa ushirikiano kwa Mahakama ya Tanzania na serikali kwa ujumla kutumia huduma hizi ili kuendeleza mapambano ya kujikinga na ugojwa wa Corona.
Kwa sasa Mahakama ya Tanzania kupitia maboresho yake, imeweka miundo - mbinu na vifaa ambavyo vitasaidia kutumia TEHAMA katika uendeshaji wa Mashauri.
TEHAMA ni silaha muhimu sana katika kuzuia mikusanyiko, kuzuia msongamano na ni mchango wa Mahakama katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Korona.
Hivi sasa, ina mifumo ifuatayo ambayo itasaidia matumizi ya TEHAMA:-
- Mfumo wa kielektroniki wa kusajili na kuratibu
Mashauri (JSDS2) uliozinduliwa na Mhe. Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli Februari 2018 wakati wa Siku ya Sheria. Mfumo huu umeunganishwa na mfumo wa malipo Serikalini (Government Electronic Payment Gateway).
- Mfumo wa kusimamia na kuwatambua Mawakili halali (TAMS).
- Mfumo wa kuhifadhi Maamuzi ya Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu (TANZLII).
- Mfumo wa video Conferencing. Wadau wa Magereza ni wanufaika wakubwa na utaratibu huu.
- Mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa majengo, watumishi na mahitaji ya Mahakama (Court Mapping - JMAP). JMAP inawezesha Viongozi wa Mahakama kupata taarifa zote muhimu hususan Mahakama zote Tanzania wakiwa pahali popote, kupitia laptop zao.
MWISHO
Nawaomba Viongozi wote wa Mahakama katika ngazi zote. Huu ndio wakati wa kuonyesha “Uongozi” kwa kuwasaidia watanzania waendelee kupata huduma za utoaji haki katika
Dunia ambayo inapata msukosuko mkubwa wa ugonjwa wa korona.
Tukumbuke kuwa karne ya 21 ni karne ya ushindani, ni karne yenye usumbufu mwingi na pia ni karne yenye nafasi nyingi zinazohitaji mabadiliko. Ugonjwa wa korona utabadilisha kabisa namna Mahakama zitakavyokuwa zinatoa haki.
Nawashukuru sana, ahsanteni kwa kunisikiliza.