This is the latest version of this Act.
Collections
Related documents
- Is amended by Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2024
- Is commenced by Notisi ya Tarehe ya kuanza Kutumika kwa Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 2023
- Repeals Tanzania Investment Act
Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.
Tanzania
Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2022
Chapter 38
- Imechapishwa katika Government Gazette 46 hadi 2 Disemba 2022
- Imeidhinishwa tarehe 27 Novemba 2022
- Ilianza 20 Februari 2023 kwa Notisi ya Tarehe ya kuanza Kutumika kwa Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 2023
- [Hili ni toleo la hati hii kutoka 22 Machi 2024.]
- [Note: This legislation was revised and consolidated as at 31 July 2002 and 30 November 2019 by the Attorney General's Office, in compliance with the Laws Revision Act No. 7 of 1994, the Revised Laws and Annual Revision Act (Chapter 356 (R.L.)), and the Interpretation of Laws and General Clauses Act No. 30 of 1972. All subsequent amendments have been researched and applied by Laws.Africa for TANZLII.]
- [Iliyorekebishwa na Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2024 (Tenda 4 ya 2024) hadi 22 Machi 2024]
Sehemu ya kwanza – Masharti ya utangulizi
1. Jina la Sheria na kuanza kutumika
Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2022 na itaanza kutumika tarehe ambayo Waziri atateua kupitia tangazo katika Gazeti la Serikali.2. Matumizi
3. Tafsiri
Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—“Bodi” maana yake ni Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo iliyoteuliwa chini ya kifungu cha 9;“cheti” maana yake ni cheti cha vivutio kilichotolewa chini ya kifungu cha 19(1);“Kituo” maana yake ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania kilichoanzishwa chini ya kifungu cha 4;“manufaa” inajumuisha nyenzo na vivutio vinavyotolewa na au kwa mujibu wa Sheria hii;“mtaji” inajumuisha mchango wa fedha taslimu, mitambo, mashine, vifaa, majengo, vipuri, ardhi, hakimiliki na mali nyingine za biashara tofauti na hadhi ambazo hazitumiki katika shughuli za kawaida za biashara na zinazoweza kudumu kwa zaidi ya miezi kumi na mbili;“mtaji wa kigeni” inajumuisha fedha zinazoweza kubadilishwa, mtambo, mashine, vifaa, vipuri, malighafi na mali nyinginezo za biashara tofauti na hadhi zinazoingia Tanzania bila malipo ya awali ya fedha za kigeni na zinazokusudiwa kuzalisha bidhaa na huduma zinazohusiana na biashara ambayo Sheria hii inatumika;“mwekezaji wa kigeni” ikiwa ni mtu binafsi maana yake ni mtu ambaye si raia wa Tanzania, na ikiwa ni kampuni, maana yake ni kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za nchi yoyote tofauti na Tanzania, kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania ambapo zaidi ya asilimia hamsini ya hisa zinamilikiwa na mtu ambaye si raia wa Tanzania, na ikiwa ni ubia, maana yake ni ubia ambapo maslahi makubwa yanamilikiwa na mtu ambaye si raia wa Tanzania;“mwekezaji wa ndani” maana yake ni mtu binafsi ambaye ni raia wa Tanzania, kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania ambapo hisa nyingi zinamilikiwa na mtu ambaye ni raia wa Tanzania, au ubia ambao maslahi makubwa yanamilikiwa na mtu ambaye ni raia wa Tanzania;“nyenzo” zinajumuisha leseni, idhini na vibali vinavyohitajika kwa ajili ya kuanzisha biashara ambazo mwekezaji atapaswa kupata kwa madhumuni ya Sheria hii;“taasisi ya kibiashara” maana yake ni kiwanda, mradi, shughuli au biashara ambayo Sheria hii inatumika au upanuzi, urekebishaji, ukarabati au uboreshaji wa kiufundi wa kiwanda, mradi, shughuli au biashara au sehemu yoyote ya biashara, ili mradi taasisi hiyo ya biashara inaendeshwa kwa madhumuni ya kupata faida na kwa misingi ya kibiashara;“uwekezaji” maana yake ni uanzishaji au umiliki wa mali mpya za biashara na inajumuisha upanuzi, urekebishaji au ukarabati wa biashara iliyopo;“vivutio” maana yake ni nafuu za kikodi, viwango vya kodi vya masharti nafuu au manufaa mengine yoyote anayoweza kupata mwekezaji chini ya sheria yoyote inayotumika kwa wakati huo; na“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji.Sehemu ya pili – Kituo cha Uwekezaji na majukumu yake
4. Kuendelea kuwepo kwa Kituo na malengo
5. Kamati ya Taifa ya Uwekezaji
6. Majukumu ya Kituo
7. Fursa za uwekezaji
Kituo kitabainisha fursa za uwekezaji zilizopo nchini na namna ya kuzifikia kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazohusika.8. Mfumo unganishi wa kielektroniki
9. Bodi
10. Mwenendo wa uendeshaji wa Bodi
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, Bodi itajiwekea utaratibu wa kuitisha na kuendesha vikao vyake.11. Kamati za Bodi
12. Mkurugenzi Mtendaji
13. Maafisa na wafanyakazi wengine wa Kituo
14. Ukomo wa uwajibikaji kwa wajumbe wa Bodi na wafanyakazi
Mjumbe, afisa au mfanyakazi mwingine wa Kituo hatawajibika kwa nafasi yake binafsi katika mashauri ya madai, kuhusiana na chochote alichotenda au kutotenda kwa nia njema katika utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii.15. Fedha za Kituo
16. Mwaka wa fedha wa Kituo
Mwaka wa fedha wa Kituo utakuwa kipindi cha mwaka mmoja utakaoishia tarehe 30 Juni.17. Hesabu, ukaguzi na taarifa
Sehemu ya tatu – Masharti yanayohusu uwekezaji
18. Kituo cha Huduma Mahala Pamoja
19. Maombi ya cheti na usajili
20. Uhai na kufutwa kwa cheti cha vivutio
21. Uratibu wa uanzishwaji wa taasisi za kibiashara
Kituo kitaratibu uanzishaji wa taasisi za kibiashara zinazosimamiwa na Sheria hii ikiwa ni pamoja na—22. Manufaa
23. Manufaa kwa uwekezaji wa kimkakati au uwekezaji maalum wa kimkakati
24. Manufaa na vivutio vinavyosimamiwa na sheria nyingine
Endapo mtu anastahili manufaa au vivutio vya kifedha au visivyo vya kifedha chini ya Sheria hii na manufaa au vivutio hivyo vinasimamiwa na sheria nyingine, manufaa au vivutio hivyo vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya sheria husika.Sehemu ya nne – Haki na Wajibu wa Serikali na Wawekezaji
25. Haki ya kusimamia uwekezaji
Serikali itakuwa na haki ya kuchukua hatua zote za kusimamia uwekezaji ili kuhakikisha kuwa shughuli za uwekezaji nchini zinaendeshwa kwa kuzingatia misingi na malengo ya Sheria hii na madhumuni ya kisera ya kijamii na kiuchumi.26. Wajibu wa mwekezaji
Mwekezaji anayetambulika na Sheria hii atakuwa na wajibu ufuatao:27. Dhamana dhidi ya kurekebishwa au kubadilishwa kwa manufaa
Kwa madhumuni ya kuweka mazingira ya uwekezaji yanayotabirika, taasisi ya kibiashara ambayo imepewa vivutio chini ya Sheria hii itakuwa na haki ya kunufaika na vivutio husika vilivyotolewa, na katika kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe ya kutolewa, vivutio hivyo havitarekebishwa au kubadilishwa kwa namna itakayomuathiri mwekezaji.28. Dhamana ya uwekezaji, uhamishaji wa mitaji, faida na gawio
Kwa kuzingatia kifungu hiki, taasisi ya kibiashara inayosimamiwa na Sheria hii inahakikishiwa kuwa, kwa kupitia benki yoyote iliyoidhinishwa na kwa aina ya fedha inayoweza kubadilishwa kwa uhuru, itaweza kuhamisha bila masharti—29. Kinga dhidi ya utaifishaji au utwaaji
29A. Hadhi ya mwekezaji wa kigeni
30. Ukomo wa idadi ya wafanyakazi wa kigeni
Kila taasisi ya kibiashara iliyopewa cheti cha vivutio chini ya Sheria hii itaruhusiwa kuwa na wafanyakazi wa kigeni kwa kuzingatia ukomo wa idadi ulioainishwa katika sheria inayosimamia masuala ya ajira kwa wageni:Isipokuwa kwamba, kwa madhumuni ya masharti ya kifungu cha 18, Kituo kitaratibu na kuwezesha upatikanaji wa haki inayotolewa chini ya kifungu hiki.31. Upatikanaji wa mikopo kwa wawekezaji wa kigeni kutoka vyanzo vya ndani.
Sehemu ya tano – Masharti ya Jumla
32. Rufaa na mapitio
32A. Utaratibu wa utatuzi wa malalamiko
33. Utatuzi wa migogoro
34. Makosa na adhabu
35. Kanuni
Waziri, baada ya kushauriwa na Bodi, anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili ya kutekeleza masharti ya Sheria hii.36. Kufutwa kwa Sheria
Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 1997 inafutwa.[Na. 26 ya Mwaka 1997]37. Masharti ya mpito
History of this document
22 March 2024 this version
31 December 2023
20 February 2023
02 December 2022
27 November 2022
Assented to
Subsidiary legislation
|
Title
|
|
|---|---|
| Government Notice 94 of 2023 |