Collections
Related documents
Tanzania
Sheria ya Ununuzi wa umma ya mwaka 2023
Chapter 410
- Imechapishwa katika Tanzania Government Gazette 40 hadi 6 Oktoba 2023
- Imeidhinishwa tarehe 29 Septemba 2023
- Ilianza 17 Juni 2023 kwa Notisi ya Tarehe ya Kuanza Kutumika kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2024
- [Hili ni toleo la hati hii kutoka 6 Oktoba 2023.]
- [Note: This legislation was revised and consolidated as at 31 July 2002 and 30 November 2019 by the Attorney General's Office, in compliance with the Laws Revision Act No. 7 of 1994, the Revised Laws and Annual Revision Act (Chapter 356 (R.L.)), and the Interpretation of Laws and General Clauses Act No. 30 of 1972. All subsequent amendments have been researched and applied by Laws.Africa for TANZLII.]
Sehemu ya Kwanza – Masharti ya utangulizi
1. Jina la Sheria na kuanza kutumika
Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na itaanza kutumika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi katika Gazeti la Serikali.2. Matumizi
3. Tafsiri
Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—“afisa masuuli” maana yake ni afisa wa umma aliyeteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Fedha za Umma au afisa wa umma aliyeteuliwa kwa sheria nyingine yoyote kusimamia fungu au ruzuku na kuwajibika kwa fedha zote zilizotumika kutoka katika fungu hilo au ruzuku;[Sura ya 348]“afisa wa umma” maana yake ni—(a)mtu yeyote anayehudumu au kufanya kazi kwenye ofisi yenye ujira katika utumishi wa umma;(b)mtu anayehudumu au kufanya kazi kama waziri katika Serikali;(c)mwajiriwa wa taasisi ya umma; au(d)mtu ambaye alikuwa afisa wa umma;“bei kikomo” maana yake ni kiwango cha chini na kiwango cha juu cha bei zitakazotumika katika ununuzi wa bidhaa, kazi za ujenzi au huduma;“bidhaa za afya” zinajumuisha dawa na vifaa tiba vilivyoidhinishwa na mamlaka ya udhibiti inayohusika na uidhinishaji wa bidhaa za afya;“bidhaa” maana yake ni malighafi, vifaa na vitu vingine vya aina mbalimbali vinavyoshikika, vikiwa katika hali ya kimiminika, ugumu au gesi, umeme, mali isiyoshikika na miliki bunifu, pamoja na huduma zinazohusiana na usambazaji wa bidhaa hizo, ili mradi thamani ya huduma hizo haizidi thamani ya bidhaa yenyewe;“Bodi” maana yake ni Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 22;“chombo chenye mamlaka” maana yake ni mtu, kikundi cha watu, wakala au chombo chenye mamlaka ya kuchukua hatua itakavyowasilishwa au kuelekezwa na Mamlaka chini ya Sheria hii;“fedha za umma” maana yake ni rasilimali fedha zilizotengwa kupitia michakato ya kibajeti kwa taasisi nunuzi, ikijumuisha Mfuko Mkuu, misaada na mikopo iliyowekwa kwa ajili ya matumizi ya taasisi nunuzi na wafadhili wa ndani au wa nje na mapato yaliyozalishwa na taasisi nunuzi;“hadidu za rejea” maana yake ni maelezo yanayotolewa na taasisi nunuzi yanayotoa tafsiri ya madhumuni, malengo na wigo wa huduma, ikijumuisha, pale itakapohitajika, njia zitakazotumika;“huduma za ushauri wa kitaalamu” maana yake ni shughuli zenye asili ya kitaalamu na kiushauri ambazo hazitoi matokeo yanayoonekana yanayoweza kupimika na hujumuisha usanifu, usimamizi, mafunzo, ushauri, ukaguzi au utengenezaji wa mifumo na huduma zinazofanana na hizo;“huduma za ushauri zisizo za kitaalam” maana yake ni ununuzi wowote mbali na ununuzi wa bidhaa, kazi za ujenzi na huduma za kitaalam;“huduma” maana yake ni huduma ya ushauri elekezi na ushauri usio wa kitaalamu;“idara ya Serikali inayojitegemea” maana yake ni idara ya Serikali ambayo haipo kwenye udhibiti wa moja kwa moja wa wizara mama ya idara hiyo;“idara” kuhusiana na wizara, mamlaka nyingine ya umma au taasisi ya umma, inajumuisha idara au kitengo chochote kwa jina lolote katika wizara, mamlaka au taasisi hiyo;“Katibu Mkuu” maana yake ni Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya masuala ya ununuzi wa umma;“kampuni ya ndani” maana yake ni kampuni ambayo sehemu kubwa ya mtaji wa hisa zake inamilikiwa na raia wa Jamhuri ya Muungano;“kazi za ujenzi” maana yake ni—(a)kazi zote za ujenzi zinazohusiana na kujenga, kujenga upya, kubomoa, kukarabati au kuboresha jengo, barabara au kiwanja cha ndege;(b)kazi nyingine zozote za ujenzi kama vile uandaaji wa eneo la kazi, uchimbaji, usimikaji, ujenzi, usimikaji mitambo au vifaa, upambaji na shughuli za ukamilishaji wa ujenzi; na(c)huduma iliyotolewa kwa zabuni na kuingiwa mkataba kwa kuzingatia misingi ya utendaji wa matokeo yanayopimika kwa kuonekana kama vile uchimbaji, uchoraji ramani, upigaji wa picha za satelaiti au uchunguzi wa miamba:Isipokuwa, mikataba inayojumuisha utoaji wa kazi za ujenzi na huduma itachukuliwa kama ni mikataba ya kazi za ujenzi ikiwa jumla ya thamani ya kazi za ujenzi ni kubwa kuliko thamani ya huduma zitakazotolewa kwenye mkataba;“kitendo cha kushurutisha” maana yake ni kitendo cha kumdhoofisha au kumdhuru au cha kutishia kumdhoofisha au kumdhuru moja kwa moja au vinginevyo, mtu yeyote au mali ya mtu kwa nia ya kushawishi kitendo kufanyika au kumshawishi mtu anayehusika na ununuzi wa umma au kuendeleza vitendo vya rushwa au vya udanganyifu;“kitendo cha udanganyifu” maana yake ni kutoa taarifa zisizo sahihi kwa lengo la kufanya ushawishi katika mchakato wa ununuzi au utekelezaji wa mkataba ambao utaleta madhara kwa Serikali au taasisi ya umma na inajumuisha vitendo vya kula njama baina ya wazabuni, kabla au baada ya wasilisho la zabuni ikilenga kuwa na bei ya zabuni ambayo si shindani na inainyima Serikali faida zitokanazo na ushindani wa wazi na huru;“kitendo cha uzuiaji” maana yake ni kitendo kinacholenga kuzuia upatikanaji wa taarifa zinazohitajika katika utekelezaji wa wajibu chini ya Sheria hii;“Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi” maana yake ni Idara au Kitengo, kutegemeana na ukubwa wa taasisi nunuzi, chenye wajibu wa utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa ununuzi na ugavi;“kumfungia mzabuni” maana yake ni kitendo cha mzabuni kuzuiwa kushiriki katika ununuzi wa umma kwa kipindi maalum;“mali ya umma” maana yake ni mali yoyote inayoshikika au isiyoshikika inayomilikiwa na taasisi ya umma inayojumuisha mali inayoshikika, ardhi, hisa au haki miliki;“mamlaka inayoingia mkataba” ina maana sawa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi;[Sura ya 103]“mamlaka ya serikali za mitaa” maana yake ni mamlaka ya serikali za mitaa iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) au Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Mji);[Sura ya 287 na 288]“Mamlaka ya Rufani” maana yake ni Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 112;“mamlaka ya uidhinishaji” maana yake ni afisa masuuli au bodi ya zabuni ya taasisi nunuzi;“Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 8;“mapendekezo ya taasisi nunuzi ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi” maana yake ni mapendekezo ya miradi ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi yanayoanzishwa na taasisi za umma na yanayohusu mipango ya kipaumbele ya Serikali;“mapendekezo ya sekta binafsi ya ubia baina yasekta ya umma na sekta binafsi” maana yake ni mapendekezo yaliyoanzishwa na upande wa sekta binafsi kwa taasisi ya umma kwa ajili ya kuamuliwa kuwa mradi wa ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi;“mchakato wa ununuzi” maana yake ni hatua zinazofuatana katika mzunguko wa ununuzi zinazojumuisha kupanga, kuchagua utaratibu, hatua za kuomba ofa kutoka kwa wazabuni, kupima na kutathmini ofa hizo, utoaji wa tuzo ya mkataba na usimamizi wa mkataba;“mchakato wa uondoshaji” maana yake ni hatua zinazofuatana katika mzunguko wa uondoshaji mali ikijumuisha uandaaji wa mpango, uchaguzi wa utaratibu utakaotumika, hatua zitakazotumika kutangaza zabuni, tathmini ya zabuni na tuzo ya mkataba;“mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa umma” maana yake ni mfumo uliojengwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Mamlaka iii kuziwezesha taasisi nunuzi kufanya shughuli za ununuzi na ugavi kielektroniki;“mikataba maalum” maana yake ni mikataba ambayo inaruhusu taasisi nunuzi kununua bidhaa, huduma au kazi za ujenzi ambazo zinahitajika kwa mwendelezo au mara kwa mara kwa makubaliano au bila ya makubaliano ya bei kwa kipindi maalum kilichokubaliwa;“miongozo” maana yake ni miongozi inayotolewa na Mamlaka chini ya Sheria hii;“mkandarasi” maana yake ni kampuni, shirika, ubia au mtu binafsi anayejihusisha na kutoa huduma katika fani za uhandisi majenzi, umeme au mitambo, au katika ujenzi au kazi za majengo za aina yoyote ikijumuisha ukarabati, na ambaye, kwa muktadha husika ni sehemu ya au anaweza kuwa sehemu ya mkataba wa ununuzi na taasisi nunuzi;“mkataba wa ununuzi” maana yake ni leseni, kibali au idhini nyingine iliyotolewa na taasisi ya umma au makubaliano yaliyoingiwa baina ya taasisi ya umma na muuzaji wa bidhaa, mkandarasi, au mshauri elekezi yanayotokana na utaratibu wa ununuzi kwa ajili ya ujenzi au kazi nyingine zinazohusiana na ujenzi au kwa ajili ya uuzaji wa bidhaa zozote au utoaji wa huduma;“Mlipaji Mkuu wa Serikali” ina maana iliyoainishwa chini ya Sheria ya Fedha za Umma;[Sura ya 348]“mshauri elekezi” maana yake ni taasisi, kampuni, shirika, asasi, ubia au mtu binafsi anayejihusisha au mwenye uwezo wa kujihusisha na biashara ya kutoa huduma katika usanifu majengo, uchumi, uhandisi, upimaji au fani yoyote ya huduma za kitaaluma na ambaye kwa muktadha husika, ni sehemu ya mkataba au anaweza kuwa sehemu ya mkataba na taasisi nunuzi;“mshirika” maana yake ni mtu ambaye—(a)ana ubia na afisa wa umma; au(b)ikiwa ni taasisi nafsi, ni msimamizi wa taasisi hiyo au afisa wa umma na mtu yeyote mwenye ushirika naye;“mtaalamu wa ununuzi” au “mtalaamu wa ugavi” maana yake ni mtu mwenye sifa za kitaaluma katika masuala ya ununuzi na ugavi kutoka katika chuo kinachotambulika na amesajiliwa na chombo kinachosimamia taaluma ya ununuzi na ugavi;“mtoa huduma” maana yake ni mtu, shirika au chombo kilichosajiliwa na kupewa leseni na mamlaka husika kutoa huduma na ambaye, kwa mujibu wa mkataba, ni sehemu ya au anaweza kuwa sehemu ya mkataba wa ununuzi na taasisi nunuzi;“mtu” inajumuisha ushirika wowote wa watu, ikiwa umesajiliwa au haujasajiliwa kama kampuni;“muuzaji wa bidhaa” maana yake ni kampuni, shirika, asasi, ubia au mtu binafsi anayeuza bidhaa na huduma zinazohusiana na bidhaa hizo na ambaye, kwa mujibu wa mkataba, ni sehemu ya au anaweza kuwa sehemu ya mkataba wa ununuzi na taasisi nunuzi;“mzabuni” maana yake ni mtu yeyote, kampuni au kikundi cha watu ambao wanashiriki au wanakusudia kushiriki kwenye mchakato wa ununuzi kwa lengo la kuwasilisha zabuni kwa ajili ya kuingia mkataba na inajumuisha muuzaji wa bidhaa, mkandarasi, mtoa huduma au mnunuzi wa mali;“mzabuni wa kigeni” maana yake ni kampuni ambayo asilimia kubwa ya mtaji wa hisa zake inamilikiwa na raia wa nchi ya kigeni;“nyaraka ya zabuni” maana yake ni nyaraka ya maandishi au kielektroniki au pendekezo la kuwaalika wazabuni kushiriki kwenye ununuzi au uondoshaji mali na inajumuisha nyaraka za mwaliko kwa wazabuni wenye sifa kwa ajili ya uchambuzi wa awali;“orodha ya bei” maana yake ni orodha inayoainisha ukomo bei ya bidhaa na huduma inayoandaliwa na kutunzwa na Mamlaka;“saini ya kidigitali” maana yake ni saini ya kielektroniki iliyokidhi vigezo vya kielektroniki vilivyoainishwa vinavyowezesha kumtambua na kumthibitisha mtia saini;“Serikali” maana yake ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;“taasisi nunuzi” maana yake ni taasisi ya umma au taasisi nyingine yoyote au kitengo kilichoanzishwa na kupewa mamlaka na Serikali kufanya shughuli za umma;“taasisi ya umma” au “mamlaka ya umma” maana yake ni—(a)wizara yoyote, idara au wakala wa Serikali;(b)kampuni yoyote au chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria au mamlaka iliyoanzishwa na Serikali;[Sura ya 212](c)kampuni yoyote iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Kampuni ambayo Serikali au wakala wa Serikali upo katika nafasi ya kufanya ushawishi wa sera za kampuni; au(d)mamlaka yoyote ya serikali za mitaa;“taasisi zinazojiendesha kibiashara” maana yake ni taasisi za umma zinazojiendesha kibiashara kama ilivyoainishwa katika Sheria inayoanzisha taasisi husika au kutambuliwa na Msajili wa Hazina kuwa zinajiendesha kibiashara;“taratibu wa ununuzi” maana yake ni taratibu zinazopaswa kuzingatiwa na taasisi nunuzi au mamlaka yoyote ya kutoa idhini inapojihusisha katika ununuzi;“thamani ya fedha” maana yake ni manufaa makubwa yanayopatikana kwenye bidhaa, kazi za ujenzi au huduma zilizonunuliwa na rasilimali zilizopo ikilinganishwa na gharama zilizotumika;“ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi” ina maana kama ilivyoainishwa chini ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi;[Sura ya 103]“uchaguzi shindani” maana yake ni njia ya ununuzi ambayo washauri elekezi au watoa huduma wanaalikwa na taasisi nunuzi kushindana katika kuwasilisha zabuni zenye bei au zisizo na bei, ambapo zabuni hizo zinapaswa kufanyiwa tathmini kwa misingi ya ubora au kwa misingi ya ubora na gharama;“uchambuzi wa sifa wa awali” maana yake ni utaratibu rasmi ambao wauzaji wa bidhaa, wakandarasi au washauri elekezi wanaalikwa kuwasilisha taarifa za rasilimali zao na uwezo wao ambapo huchambuliwa kabla ya mwaliko wa zabuni kwa kuzingatia vigezo vya msingi vilivyowekwa kuhusu uzoefu, rasilimali, uwezo na hali ya kifedha;“ugavi” maana yake ni utaratibu unaotumiwa na taasisi nunuzi kuwezesha upatikanaji, upokeaji, usambazaji, uhifadhi, utunzaji, utumiaji wa vifaa, bidhaa na huduma kwa idara tumizi;“ugavi wa kielektroniki” maana yake ni ugavi unaofanywa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kwa mujibu wa Sheria hii;“uhakiki wa sifa za mzabuni” maana yake ni tathmini ya kina inayofanywa baada ya tathmini ya zabuni kukamilika kabla ya kutolewa tuzo ya mkataba, ili kuthibitisha endapo mzabuni aliyekidhi vigezo na mwenye bei ya chini zaidi au mwenye bei ya juu zaidi katika zabuni za ukusanyaji mapato ana uzoefu, uwezo na rasilimali za kutekeleza mkataba kwa ufanisi;“ununuzi wa dharura” maana yake ni ununuzi wa bidhaa, kazi za ujenzi au huduma ili kukidhi hali ya dharura ambao hauwezi kufanyika kwa mchakato wa kawaida wa ununuzi;“ununuzi wa kielektroniki” maana yake ni ununuzi wa umma unaofanywa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kwa mujibu wa Sheria hii;“ununuzi” maana yake ni kununua, kupanga, kukodisha, kununua kwa kukodisha, au kupata bidhaa, kazi za ujenzi au huduma yoyote kwa taasisi nunuzi na inajumuisha kazi zote zinazohusisha upatikanaji wa bidhaa, kazi za ujenzi au huduma ikijumuisha kutambua na kuandaa mahitaji, uchaguzi na mwaliko wa wazabuni, maandalizi ya mikataba, tuzo na usimamizi wa mikataba;“uondoshaji mali” maana yake ni uhamishaji wa umiliki wa mali za umma zikiwemo miliki bunifu, haki miliki, sifa ya kibiashara, haki nyingine zozote za taasisi nunuzi au taasisi inayoondosha mali kwa njia ya zabuni kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii;“usimamizi wa mnyororo wa ugavi” hujumuisha shughuli zote za utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za mnyororo wa ugavi ikijumuisha usanifu, utambuzi wa mahitaji, uandaaji wa mpango, ununuzi, upokeaji, uhifadhi, utunzaji, usambazaji, usimamizi wa mikataba, matumizi na uondoshaji mali kwa lengo la kupata thamani ya fedha iliyokusudiwa na taasisi nunuzi;“usimamizi wa ugavi” maana yake ni uratibu na utekelezaji wenye unafuu na wenye ufanisi wa—(a)mpangilio wa ghala, uhifadhi, udhibiti wa orodha ya bidhaa na uhifadhi wa bidhaa;(b)usambazaji wa bidhaa ikiwemo usafirishaji, utunzaji, ugomboaji na uondoshaji na uhakiki na uondoshaji katika forodha na bandari;(c)uhakiki na uhesabu mali;(d)uondoshaji mali, uchakataji wa mali kwa mara nyingine, uhamishaji wa mali, upigaji mnada na uhifadhi;“utoaji wa taarifa za uongo” maana yake ni uwasilishaji wa taarifa zisizo za kweli unaofanywa na mtu kwa mtu mwingine kwa nia ya kudanganya wakati akijua kuwa taarifa hizo ni za uongo;“vifaa tiba” maana yake itakuwa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba;[Sura ya 219]“vigezo msawazo” maana yake ni maelezo ya bidhaa, kazi za ujenzi au huduma yoyote kwa kurejea aina, ubora, uimara, uhalisia, muundo, wingi, upana, uzito, daraja, umadhubuti, chanzo, umri au sifa nyingine au kwa kurejea kitu chochote ambacho aukwa namna yoyote ambayo, bidhaa, huduma au kazi za ujenzi zinaweza kutengenezwa, kuzalishwa, kuchakatwa, kuboreshwa, kujengwa au kusimikwa;“vitendo vya kula njama” maana yake ni mpango kati ya pande mbili au zaidi zikiwa na ufahamu au bila kuwa na ufahamu wa upande au pande nyingine kwa madhumuni ya kufanikisha lengo lisilo halali, ikiwa ni pamoja na kushawishi isivyo halali vitendo vya mtu mwingine;[Sura ya 329]“vitendo vya rushwa” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa;[Sura ya 61]“vyombo vya ulinzi na usalama” ina maana sawa kama ilivyoainishwa chini ya Sheria ya Baraza la Ulinzi la Taifa;“Wakala” maana yake ni Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini;“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya ununuzi wa umma;“zabuni” maana yake ni ofa, pendekezo au ofa ya bei iliyowasilishwa na muuzaji wa bidhaa, mtoa huduma, mkandarasi au mshauri elekezi katika kuitikia ombi la taasisi nunuzi;“zabuni iliyoshinda” maana yake ni zabuni iliyofanyiwa tathmini na kuchaguliwa na taasisi nunuzi kuwa—(a)yenye gharama ya chini zaidi iliyotathminiwa na uwezo wa kutekeleza mkataba, ikiwa njia ya ununuzi iliyotumika ni ya zabuni shindani;(b)ndio iliyokidhi zaidi mahitaji ya taasisi nunuzi endapo ununuzi unafanyika kwa njia ya ushindani wa bei, ununuzi kutoka kwa mzabuni mmoja, uchaguzi shindani au pale ambapo bidhaa au huduma za thamani ndogo zinanunuliwa; au(c)nabei ya juu zaidi iliyotathminiwa;“zabuni shindani” maana yake ni njia ya ununuzi ambayo wauzaji wa bidhaa, wakandarasi, watoa huduma au washauri elekezi wanaalikwa na taasisi nunuzi kushindana kwa kuwasilisha zabuni zenye bei kwa ajili ya bidhaa, kazi za ujenzi au huduma;“zabuni yenye bei ya chini zaidi iliyofanyiwa tathmini” maana yake ni zabuni yenye bei ya chini zaidi baada ya kuzingatia vigezo vyote muhimu vya upimaji vilivyokokotolewa ili mradi vigezo hivyo vimeainishwa katika nyaraka za zabuni; na“zabuni yenye bei ya juu zaidi iliyofanyiwa tathmini” maana yake ni zabuni yenye bei ya juu zaidi iliyotolewa na mzabuni baada ya kufanyiwa tathmini inayohusu ukusanyaji wa mapato au uondoshaji wa mali ambayo imeonekana kuwa na bei ya juu zaidi baada ya kuzingatia vigezo vyote muhimu vilivyoainishwa katika nyaraka za zabuni.4. Wajibu wa Kimataifa
5. Misingi na viwango vya jumla vya ununuzi, ugavi na uondoshaji mali
Sehemu ya Pili – Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma
6. Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma
7. Majukumu ya Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma
Majukumu ya Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma yatakuwa—Sehemu ya Tatu – Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma
8. Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma
9. Malengo ya Mamlaka
Malengo ya Mamlaka yatakuwa ni—10. Majukumu ya Mamlaka
Majukumu ya Mamlaka yatakuwa ni—11. Wigo wa uchunguzi unaofanywa na Mamlaka
12. Uanzishaji wa uchunguzi
Uchunguzi wowote utakaofanywa kwa mujibu wa kifungu cha 11 unaweza kufanywa na Mamlaka kwa utashi wake au kutokana na taarifa zilizowasilishwa kwake, ikiwa kwa maoni yake, uchunguzi huo unapaswa kufanyika.13. Ushahidi
14. Katazo la utoaji wa baadhi ya taarifa
15. Utaratibu wa uchunguzi
Katika kufanya uchunguzi, Mamlaka inaweza kutumia utaratibu wowote itakayoona unafaa kulingana na mazingira ya suala husika na kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii.16. Utaratibu baada ya uchunguzi
17. Hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi wa umma
18. Taratibu za uendeshaji wa Mamlaka
Taratibu za uendeshaji wa Mamlaka au kamati zake hazitachukuliwa kuwa batili kwa kigezo cha kutokuwepo kwa utaratibu ulioainishwa.19. Mamlaka ya Mamlaka
20. Usitishaji wa michakato ya ununuzi
21. Hatua baada ya mapendekezo ya Mamlaka
22. Bodi ya Wakurugenzi
23. Kamati za Bodi ya Wakurugenzi
24. Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu
25. Wakurugenzi, washauri elekezi na watumishi wengine wa Mamlaka
26. Fedha za Mamlaka
27. Vitabu vya hesabu
28. Ukaguzi wa hesabu
29. Mpango kazi wa mwaka na bajeti
30. Taarifa ya mwaka ya tathmini ya utendaji kazi wa ununuzi wa umma na thamani halisi ya fedha
Ifikapo au kabla ya tarehe 30 Machi kila mwaka, au kwa tarehe nyingine ambayo Rais ataelekeza, Mamlaka itawasilisha kwa Rais taarifa ya mwaka ya tathmini ya utendaji kazi wa ununuzi wa umma, ugavi na uondoshaji mali na thamani halisi ya fedha itakayo jumuisha—31. Taarifa ya mwaka
Sehemu ya Nne – Mpangilio wa kitaasisi katika ununuzi na ugavi
32. Bodi za zabuni
33. Taarifa kwa Mamlaka kuhusu muundo wa bodi ya zabuni
34. Majukumu ya bodi za zabuni
Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 32, majukumu ya bodi ya zabuni yatakuwa ni—35. Mamlaka ya kuidhinisha bajeti
36. Mamlaka ya bodi ya zabuni
Katika kutekeleza mamlaka yake chini ya Sheria hii, bodi za zabuni zinaweza—37. Tuzo ya mikataba
38. Majukumu na mamlaka ya afisa masuuli
39. Uanzishwaji na muundo wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
40. Majukumu ya Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi—41. Idara tumizi
42. Kamati ya Tathmini
43. Uhuru wa majukumu na mamlaka
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, afisa masuuli, bodi ya zabuni, Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, idara tumizi na kamati za tathmini zitatekeleza majukumu na mamlaka yake bila kuingiliwa.44. Ukasimishaji wa mamlaka ya afisa masuuli
45. Ununuzi kupitia taasisi nyingine
46. Taratibu za ununuzi kwa ajili ya Mamlaka na Mamlaka ya Rufani
47. Kutokubaliana katika maamuzi
48. Usiri wa nyaraka
Sehemu ya Tano – Taratibu mbalimbali za ununuzi wa umma
49. Ununuzi katika taasisi zinazojiende sha kibiashara
Mashirika na taasisi za umma zinazojiendesha kibiashara zitafanya ununuzi, ugavi au uondoshaji mali za umma kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa katika kanuni.50. Wajibu wa taasisi nunuzi
51. Uidhinishaji wa mpango wa ununuzi wa mwaka
52. Ununuzi kupitia mikataba maalumu
53. Sifa za wazabuni
54. Taratibu za uchambuzi wa sifa wa awali
55. Uhakiki wa sifa za mzabuni
56. Upendeleo wa kitaifa
57. Upendeleo wa
58. Ushiriki wa kampuni za ndani na wataalamu katika mikataba ya ushauri elekezi
59. Matumizi ya
Wakati wa kutoa upendeleo kwenye kazi za wataalamu wa ndani katika mikataba ya kazi za ujenzi na huduma zisizo za kitaalamu ujenzi au huduma zisizo za kitaalam, taasisi nunuzi itafuata miongozo itakayotolewa na Mamlaka, na itazingatia—60. Upendeleo kwa bidhaa za ndani
61. Kujenga uwezo wa watu na kampuni za ndani
62. Uingiaji wa ushirika au mikataba midogo na kampuni za ndani
63. Umiliki wa mtaji wa hisa
Bila kujali masharti mengine yoyote yanayoeleza vinginevyo, kampuni za ndani zilizorejewa chini ya vifungu vya 58 na 61 zitapaswa kuwa na mtaji wa hisa ambao wote unamilikiwa na raia wa Jamhuri ya Muungano.64. Upendeleo kwa makundi maalum ya kijamii
65. Ununuzi kutoka kwa Wakala
Taasisi nunuzi itafanya ununuzi kutoka kwa Wakala kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa katika kanuni.66. Lugha
Nyaraka za tathmini ya awali na nyaraka za zabuni zitaandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kingereza na zabuni zitaitishwa kwa yoyote kati ya lugha hizo.67. Dhamana za zabuni
68. Kukataliwa kwa zabuni
69. Kukubaliwa kwa zabuni na mkataba kuwa na nguvu ya kisheria
70. Ushuhudiaji wa utiajisaini wa mkataba
71. Kumbukumbu na taarifa
72. Kufungiwa kwa mzabuni
Sehemu ya Sita – Njia na michakato ya ununuzi
73. Ununuzi kwa njia ya kielektroniki
74. Bei kikomo
75. Uchaguzi wa njia za ununuzi
76. Matumizi ya rasilimali za ndani
77. Ununuzi wa dharura
78. Ununuzi wa moja kwa moja kutoka kwa mzalishaji, wakala au mtoa huduma
79. Viwango vya ununuzi vilivyoidhinish wa
80. Ununuzi wa
81. Zabuni shindani
Taasisi nunuzi inayokusudia kuanzisha zabuni shindani itawapa wazabuni wote wenye sifa taarifa za kutosha na kwa wakati kuhusu mahitaji ya taasisi nunuzi na fursa sawa ya kuwasilisha zabuni.82. Bidhaa za afya
83. Mwaliko wa zabuni na matangazo
84. Utoaji wa
85. Maudhui ya nyaraka za zabuni
86. Uhalali wa zabuni na dhamana ya zabuni
Taasisi nunuzi itawataka wazabuni kuhakikisha zabuni na dhamana za zabuni husika ni halali kwa vipindi vilivyoainishwa kwenye nyaraka za zabuni, kwa kiwango kitakachotosha kuiwezesha taasisi nunuzi kukamilisha ulinganifu na tathmini ya zabuni, uidhinishaji wa mapendekezo, utoaji wa taarifa ya tuzo na kusainiwa kwa mkataba.87. Vigezo vya tathmini
88. Kupokelewa na kufunguliwa kwa zabuni
89. Tathmini na ulinganifu wa zabuni
90. Uidhinishaji wa tuzo ya mkataba
Bodi ya zabuni au afisa masuuli atapitia taarifa ya tathmini na mapendekezo ya Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na anaweza—91. Majadiliano na utoaji wa tuzo ya mikataba
92. Uchaguzi wa washauri elekezi
Sehemu ya Saba – Usimamizi wa mikataba
93. Wajibu wa kusimamia
94. Udhibiti wa gharama, ubora na muda katika mikataba ya ununuzi
95. Mabadiliko au marekebisho
96. Malipo ya awali
97. Uvunjaji wa mkataba
98. Ufungaji wa mkataba
Sehemu ya Nane – Usimamizi wa ugavi
99. Upokeaji na uwekaji kumbukumbu wa bidhaa, vifaa au mali
100. Wajibu wa taasisi nunuzi katika usimamizi wa bidhaa, vifaa au mali
101. Usimamizi wa bidhaa, vifaa au mali
102. Usambazaji wa bidhaa na vifaa
103. Udhibiti wa hasara na udanganyifu katika bidhaa, vifaa na mali
Taasisi nunuzi itaweka na kuhakikisha uzingatiaji wa taratibu za udhibiti, ugunduzi na uwajibikaji kwa hasara na vitendo vya udanganyifu kwa bidhaa, vifaa au mali zilizopokelewa kama itakavyoainishwa katika Sheria ya Fedha za Umma.[Sura ya 348]104. Miongozo ya usimamizi wa bidhaa, vifaa au mali
Taasisi nunuzi itazingatia miongozo itakayotolewa na Mlipaji Mkuu wa Serikali inayohusu usimamizi wa bidhaa, vifaa na mali chini ya Sheria ya Fedha zaUmma.[Sura ya 348]Sehemu ya Tisa – Ununuzi chini ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi
105. Wigo, matumizi na idhini
106. Uchaguzi wa mshauri au meneja wa mradi
Endapo mshauri au meneja wa mradi anatakiwa kuteuliwa kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa utekelezaji wa ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi unaenda vizuri, uchaguzi wa mshauri au meneja huyo utafanyika kwa mujibu wa taratibu zilizoainishwa kwenye kanuni zilizotengenezwa chini ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.[Sura ya 103]Sehemu ya Kumi – Makatazo
107. Udanganyifu na rushwa
108. Vitendo vinavyoshawishi mtumishi wa umma
109. Ufichuaji wa malipo yaliyofanywa kwa njia ya kamisheni
110. Vitendo vya wakurugenzi, wafanyakazi au mawakala
111. Ufunguaji wa mashauri ya jinai
Hatua zilizoainishwa na Sheria hii hazitazuia uanzishwaji wa mashauri yajinai kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa au sheria nyingine yoyote dhidi ya mtu yeyote anayetekeleza majukumu au anayetumia mamlaka chini ya Sheria hii au kanuni chini ya Sheria hii.[Sura ya 16 na 329]Sehemu ya Kumi na moja – Utatuzi wa migogoro
112. Mamlaka ya Rufani
113. Uteuzi wa Katibu Mtendaji
114. Watumishi wa Mamlaka ya Rufani
Mamlaka ya Rufani itaajiri watumishi kwa idadi na kada kwa kuzingatia muundo ulioidhinishwa na ikama.115. Fedha za Mamlaka ya Rufani
116. Ukaguzi wa hesabu
117. Mpango kazi wa usimamizi wa mwaka na bajeti
118. Taarifa ya mwaka
119. Haki ya mapitio
120. Utatuzi wa malalamiko au migogoro kwa maafisa masuuli
121 Rufaa au malalamiko kwa Mamlaka ya Rufani
122. Nyongeza ya muda wa kuwasilisha malalamiko, mgogoro au rufaa
Mamlaka ya Rufani inaweza kuongeza muda ulioainishwa chini ya kifungu cha 121(1) na (2) endapo imejiridhisha kwamba kushindwa kwa mhusika kuwasilisha malalamiko, mgogoro au rufaa kulisababishwa na kutokuwepo kwake ndani ya Jamhuri ya Muungano, ugonjwa au sababu nyingine ya msingi, kwa kuzingatia vigezo na masharti kama yanavyoweza kuainishwa katika kanuni.123. Taratibu zinazotumika katika mienendo ya mapitio
124. Kusitishwa kwa mchakato wa ununuzi
125. Mapitio ya kimahakama
Sehemu ya Kumi na mbili – Masharti ya jumla
126. Kanuni za maadili
127. Kinga dhidi ya uwajibikaji
Mjumbe yeyote au mwajiriwa yeyote wa Mamlaka au Mamlaka ya Rufani hatafunguliwa shauri, madai au kuwajibishwa kwa kitendo au jambo ikiwa kitendo au jambo husika lilitendwa au kutotendwa kwa nia njema katika utekelezaji wa majukumu yake kama mjumbe au mwajiriwa wa Mamlaka au Mamlaka ya Rufani.128. Makosa
129. Kanuni
130. Miongozo
Mamlaka itatoa miongozo kwa ajili ya utekelezaji bora wa malengo au majukumu chini ya Sheria hii.131. Kufutwa kwa Sheria na masharti ya mwendelezo
History of this document
31 December 2023
Chapter 410
Revised Laws 2023
Consolidation
06 October 2023 this version
29 September 2023
Assented to
17 June 2023
Cited documents 0
Documents citing this one 3
Judgment
3|
Leave to seek judicial review of a procurement decision granted where the applicant showed an arguable case and timely filing.
Judicial review – Application for leave – Public procurement – Exhaustion of local remedies – Limitation period – Prima facie case for review.
|
|
A procurement authority may initiate debarment suo motu and is not bound by the 28‑day limit applicable to procuring entities' proposals.
* Public procurement – Debarment – Distinction between debarment proposals submitted by procuring entities/third parties and debarment initiated suo motu by the regulatory Authority – Regulation 98(1) time limit applies to proposals by others, not Authority‑initiated debarments.* Administrative law – Judicial review – Illegality and procedural fairness – Right to be heard and admissibility of documents produced in appellate proceedings.* Section 125(2)(b)–(3) Public Procurement Act – Case stated by Attorney General and weight of AG opinion.
|
|
Applicants lacked locus standi to sue on a lease that did not name them; application dismissed.
• Civil procedure – Preliminary objections – jurisdiction vs. substantive suit – abstention where determination may affect main proceedings.
• Locus standi – interest in contract – a person cannot sue on a contract in which they are not a party or have not shown a legal interest.
• Res judicata/overtaken by events – issues arising from prior proceedings should be raised in the substantive suit.
|