Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.
Tanzania
Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi, 2025
Tenda 6 ya 2025
- Imechapishwa katika Government Gazette Act Supplement 6 hadi 30 Juni 2025
- Imeidhinishwa tarehe 4 Machi 2025
- Ilianza tarehe 30 Juni 2025
- [Hili ni toleo la hati hii kama ilivyokuwa kutoka 30 Juni 2025 hadi 30 Juni 2025.]
Sehemu ya kwanza – Masharti ya utangulizi
1. Jina
Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi ya Mwaka 2025.2. Matumizi
3. Tafsiri
Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo:“Bodi” maana yake ni Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka iliyoteuliwa chini ya kifungu cha 8;“cheti” maana yake ni cheti cha uwekezaji kinachotolewa na Mamlaka kwa mwekezaji anayewekeza katika eneo lililo nje ya eneo maalumu la kiuchumi kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii;“eneo la forodha” maana yake ni eneo lililoteuliwa kama eneo la forodha kwa mujibu wa sheria inayosimamia masuala ya forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki;“eneo maalumu la kiuchumi” maana yake ni eneo la ardhi lililoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 26;“leseni” maana yake ni idhini iliyotolewa na Mamlaka kwa ajili ya uendelezaji wa miundombinu, uendeshaji au uzalishaji katika eneo maalumu la kiuchumi;“Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 4;“mamlaka ya forodha” maana yake ni Mamlaka ya Mapato Tanzania;“mtaji” inajumuisha mchango wa fedha taslimu, mitambo, mashine, vifaa, majengo, vipuri, ardhi, hakimiliki na mali nyingine za biashara tofauti na hadhi ambazo hazitumiki katika shughuli za kawaida za biashara na zinazoweza kudumu kwa zaidi ya miezi kumi na mbili;“mtaji wa kigeni” inajumuisha fedha zinazoweza kubadilishwa, mtambo, mashine, vifaa, vipuri, malighafi na mali nyinginezo za biashara tofauti na hadhi zinazoingia Tanzania bila malipo ya awali ya fedha za kigeni na zinazokusudiwa kuzalisha bidhaa na huduma zinazohusiana na biashara inayosimamiwa na Sheria hii;“mwekezaji wa kigeni” maana yake ni—(a)mtu binafsi ambaye si raia wa Tanzania;(b)kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za nchi yoyote tofauti na Tanzania inayofanya uwekezaji wa moja kwa moja nchini;(c)kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania ambapo asilimia hamsini au zaidi ya hisa zinamilikiwa na mtu ambaye si raia wa Tanzania; au(d)ikiwa ni ubia, ni ubia ambao sehemu kubwa ya maslahi inamilikiwa na mtu ambaye si raia wa Tanzania;“mwekezaji wa ndani” maana yake ni mtu binafsi ambaye ni raia wa Tanzania, kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania ambayo sehemu kubwa ya hisa inamilikiwa na raia wa Tanzania, au ubia ambao sehemu kubwa ya maslahi inamilikiwa na raia wa Tanzania;“uwekezaji” maana yake ni mchango wa mtaji wa ndani au wa kigeni kutoka kwa mwekezaji unaohusisha uanzishaji au ununuzi wa mali mpya kwa ajili ya biashara, na inajumuisha upanuzi au ukarabati wa biashara iliyopo;“vivutio” maana yake ni misamaha ya kodi, nafuu za kodi au manufaa mengine yoyote anayoweza kupata mwekezaji chini ya sheria yoyote inayotumika; na“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji.Sehemu ya pili – Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania
4. Kuanzishwa kwa Mamlaka
5. Malengo ya uanzishwaji wa Mamlaka
Mamlaka inaanzishwa kwa lengo la kuwa sehemu ya huduma mahala pamoja kwa wawekezaji na itakuwa ndicho chombo kikuu cha Serikali cha kuratibu, kuhimiza, kuhamasisha na kuwezesha uwekezaji Tanzania na kuishauri Serikali kuhusu sera ya uwekezaji.6. Majukumu ya Mamlaka
Mamlaka itatekeleza majukumu yafuatayo:7. Kamati ya Taifa ya Maendeleo ya Uwekezaji
8. Bodi ya Mamlaka
9. Majukumu na mamlaka ya Bodi
10. Mkurugenzi Mkuu
11. Watumishi wa Mamlaka
Sehemu ya tatu – Uwezeshaji wa uwekezaji
12. Kituo cha Huduma Mahala Pamoja
13. Huduma zinazotolewa nje ya Kituo cha Huduma Mahala Pamoja
14. Mfumo unganishi wa kielektroniki
15. Usajili wa wawekezaji
16. Maombi ya cheti au leseni
17. Maombi ya cheti au leseni
18. Kubadili au kuacha uwekezaji
19. Vivutio vya uwekezaji
20. Orodha ya vivutio vya uwekezaji
21. Mwekezaji wa kimkakati
22. Fursa kwa mwekezaji wa ndani
Waziri, kwa kushauriana na Waziri mwenye dhamana ya fedha, anaweza kubainisha maeneo mahsusi ambayo wawekezaji wa ndani wanaweza kupewa vivutio kwa kuzingatia Sheria husika.23. Benki ya ardhi
24. Usimamizi wa ardhi ya uwekezaji
Sehemu ya nne – Maeneo maalumu ya kiuchumi
25. Uanzishaji wa maeneo maalumu ya kiuchumi
26. Utaratibu wa uanzishaji wa maeneo maalumu ya kiuchumi
27. Masuala ya forodha katika eneo maalumu la kiuchumi
28. Uingizaji na utoaji wa huduma na bidhaa katika maeneo maalumu ya kiuchumi
29. Usimamizi wa eneo maalumu la kiuchumi
30. Watoa huduma katika eneo maalumu la kiuchumi
Sehemu ya tano – Haki na wajibu wa Serikali na wawekezaji
31. Haki ya kusimamia uwekezaji
32. Wajibu wa mwekezaji
Mwekezaji atakuwa na wajibu ufuatao:33. Dhamana ya uhamishaji wa mitaji, faida na gawio
34. Kinga dhidi ya utaifishaji au utwaaji
35. Fursa sawa kwa mwekezaji wa kigeni
36. Ukomo wa idadi ya wafanyakazi wa kigeni
Mwekezaji ataruhusiwa kuajiri wafanyakazi wa kigeni kwa kuzingatia ukomo wa idadi ulioainishwa katika sheria inayosimamia masuala ya ajira kwa wageni.37. Upatikanaji wa mikopo kwa wawekezaji wa kigeni kutoka vyanzo vya ndani
Sehemu ya sita – Ushughulikiaji wa malalamiko na utatuzi wa migogoro
38. Utaratibu wa kushughulikia malalamiko
39. Rufaa
40. Utatuzi wa migogoro
Sehemu ya saba – Masharti ya fedha
41. Vyanzo vya fedha za Mamlaka
Vyanzo vya fedha za Mamlaka vitajumuisha—42. Bajeti ya Mamlaka
43. Hesabu na ukaguzi
44. Taarifa ya mwaka
Sehemu ya nane – Masharti ya jumla
45. Makosa na adhabu
46. Adhabu ya jumla
Mtu yeyote ambaye atakiuka masharti ya Sheria hii ambapo adhabu haikuainishwa, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni mbili na isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miaka miwili au vyote.47. Kinga dhidi ya uwajibikaji binafsi
Mjumbe wa Bodi, Mkurugenzi Mkuu au afisa wa Mamlaka hatafunguliwa shauri, madai au kuwajibishwa kwa nafasi yake binafsi kwa kitendo au jambo alilotenda au kutotenda kwa nia njema katika utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii.48. Rejesta ya uwekezaji
Mamlaka itatunza rejesta ya uwekezaji itakayokuwa na taarifa kuhusu wawekezaji wanaohudumiwa na Mamlaka, shughuli za uwekezaji zinazofanyika nchini na taarifa nyingine kadiri Bodi itakavyoamua.49. Matumizi ya Sheria nyingine
50. Kanuni
Waziri anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya Sheria hii.51. Masharti ya mpito na kufutwa kwa Sheria
Sehemu ya tisa – Marekebisho ya Sheria mbalimbali
(a) – Marekebisho ya Sheria ya Ardhi, (Suraya 113)
52. Ufafanuzi
Sehemu Ndogo hii itasomwa pamoja na Sheria ya Ardhi ambayo hapa imerejewa kama “Sheria kuu”.[Sura ya 113]53. Marekebisho ya jumla
Sheria kuu inafanyiwa marekebisho ya jumla—54. Marekebisho ya kifungu cha 2
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 2 kwa kufuta na kuandika upya tafsiri ya msamiati “foreign company” kama ifuatavyo:55. Marekebisho ya kifungu cha 6
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 6(1) kwa—56. Marekebisho ya kifungu cha 19
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 19(2)—(b) – Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Ajira kwa Raia wa Kigeni, (Suraya 436)
57. Ufafanuzi
Sehemu Ndogo hii itasomwa pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Ajira kwa Raia wa Kigeni ambayo hapa imerejewa kama “Sheria kuu”.[Sura ya 436]58. Marekebisho ya kifungu cha 19
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 19 kwa kufuta maneno “Tanzania Investment Centre and Export Processing Zones Authority” yanayoonekana katika kifungu kidogo cha (1) na (3) na badala yake kuweka maneno “Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority”.(c) – Sheria ya Kodi ya Mapato, (Suraya 332)
59. Ufafanuzi
Sehemu Ndogo hii itasomwa pamoja na Sheria ya Kodi ya Mapato ambayo hapa imerejewa kama “Sheria kuu”.[Sura ya 332]60. Marekebisho ya kifungu cha 3
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 3 kwa kufuta maneno “Tanzania Investment Act” katika tafsiri ya msamiati “strategic investor” na badala yake kuweka maneno “Investment and Special Economic Zones Act”.61. Marekebisho ya kifungu cha 10
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 10(3)(b) kwa kufuta na kuandika upya aya ndogo ya (iii) kama ifuatavyo:62. Marekebisho ya kifungu cha 143
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 143(4) kwa kufuta maneno “Tanzania Investment Centre under the Tanzania Investment Act” na badala yake kuweka maneno “Tanzania Investment and Economic Zones Authority under the Investment and Special Economic Zones Act”.63. Marekebisho ya Jedwali la Pili
Sheria kuu inarekebishwa katika Jedwali la Pili katika kivuo cha aya (o) kwa kufuta maneno “category B investor in the Special Economic Zone as provided in the Special Economic Zones Act” na badala yake kuweka maneno “an investor in the special economic zone producing for sale into the customs territory”.(d) – Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, (Suraya 148)
64. Ufafanuzi
Sehemu Ndogo hii itasomwa pamoja na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ambayo hapa imerejewa kama “Sheria kuu”.[Sura ya 148]65. Marekebisho ya kifungu cha 6
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 6 kwa kufuta na kuandika upya kifungu kidogo cha (1A) kama ifuatavyo:(e) – Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, (Sura ya 147)
66. Ufafanuzi
Sehemu Ndogo hii itasomwa pamoja na Sheria ya Ushuru wa Bidhaa ambayo hapa imerejewa kama“Sheria kuu”.[Sura ya 147]67. Marekebisho ya kifungu cha 128
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 128 kwa kufuta na kuandika upya kifungu kidogo cha (2B) kama ifuatavyo:(f) – Sheria ya Tozo za Barabara na Mafuta, (Sura ya 220)
68. Ufafanuzi
Sehemu Ndogo hii itasomwa pamoja na Sheria ya Tozo za Barabara na Mafuta ambayo hapa imerejewa kama “Sheria kuu”.[Sura ya 220]69. Marekebisho ya kifungu cha 8
Sheria kuu inarekebishwa katika kifungu cha 8 kwa kufuta na kuandika upya kifungu kidogo cha (2) kama ifuatavyo:History of this document
01 July 2025 amendment not yet applied
Amended by
Finance Act, 2025
30 June 2025 this version
04 March 2025
Assented to