Collections
Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.
Tanzania
Law of Marriage Act
Kanuni za Ndoa Kuhusu Kazi za Manaibu Wasajili Wakuu wa Ndoa na Talaka, 1975
Tangazo la Serikali 260 ya 1975
- Imechapishwa katika Tanzania Government Gazette
- Ilianza tarehe 5 Disemba 1975
- [Hili ni toleo la hati hii katika 31 Julai 2002.]
- [Note: This legislation was revised and consolidated as at 31 July 2002 and 30 November 2019 by the Attorney General's Office, in compliance with the Laws Revision Act No. 7 of 1994, the Revised Laws and Annual Revision Act (Chapter 356 (R.L.)), and the Interpretation of Laws and General Clauses Act No. 30 of 1972. All subsequent amendments have been researched and applied by Laws.Africa for TANZLII.]
1.
Kanuni hizi ziitwe kanuni za Ndoa Kuhusu Kazi za Manaibu Wasajili Wakuu wa Ndoa na Talaka.2.
Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka aweza kumpa Naibu Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka, aliyeteuliwa chini ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 3 cha Sheria ya Ndoa kufanya zile kazi zote za Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka alizopewa chini ya Sheria hiyo iliyotajwa au Sheria tanzu yoyote iliyofanywa kwa mujibu wa Sheria hiyo.3.
Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka aweza kumpa Naibu Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka uongozi wa kawaida au wa aina maalum kumsaidia huyo Naibu Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka katika kutenda yoyote kati ya kazi zake hizo na huyo Naibu Msajili Mkuu itabidi atekeleze kila uongozi kama huo.History of this document
31 July 2002 this version
Consolidation
05 December 1975
Commenced