Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Mtera ya mwaka 2023

Government Notice 307 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Mtera ya mwaka 2023
Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Mtera ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 307 ya 2023

  • Imechapishwa katika Gazette of the United Republic of Tanzania 15 hadi 28 Aprili 2023
  • Imeidhinishwa tarehe 17 Machi 2023
  • Ilianza tarehe 28 Aprili 2023
  • [Hili ni toleo la hati hii kutoka 28 Aprili 2023.]
[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Mtera ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mipangokina ya eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P1 yenye majira - nukta 808394MS, 9210769KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 1.16 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P2 yenye majira - nukta 809139MS, 9209853KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita1.08 kwa kufuata korongo hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P3 yenye majira - nukta 809682MS,9209005KZ, baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 5.0 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P4 yenye majira - nukta 805304MS, 9206386KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 1.56 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P5 yenye majira - nukta 804834MS, 9207719KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P6 yenye majira - nukta 803782MS, 9209148KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini-Mashariki kwa umbali wa kilomita 4.8 hadi ulipoanzia”

History of this document

28 April 2023 this version
Published in Gazette of the United Republic of Tanzania 15
Commenced
17 March 2023
Assented to
To the top