Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Bulengahasi - Katoro ya mwaka 2023

Government Notice 313 of 2023

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Bulengahasi - Katoro ya mwaka 2023

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Bulengahasi - Katoro ya mwaka 2023

Tangazo la Serikali 313 ya 2023

[Imetengenezwa chini ya kifungu cha 81 na 231]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Bulengahasi - Katoro ya mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji la mpango wa urasimishaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpangokina wa eneo

Mipangokina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Jedwali (Limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la urasimishaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 379615MS, 9664994KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KZ107°MS kwa umbali wa kilomita 2.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upiamji namba B yenye majira - nukta 378871MS, 9665571KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa KZ147°MG kwa umbali wa kilomita 0.07 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 378518MS, 9665789KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ164°MG kwa umbali wa kilomita 0.09 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 378315MS, 9665430KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ119°MG kwa umbali wa kilomita 1.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira - nukta 377543MS, 9666231KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS108°MG kwa umbali wa kilomita 2.4 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba F yenye majira - nukta 377565MS, 9667487KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa KS135° kwa umbali wa kilomita 0.5 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba G yenye majira - nukta 380043MS, 9668496KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS73°MS kwa umbali wa kilomita 0.7 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba H yenye majira - nukta 380846MS, 9667906KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KZ281°MS kwa umbali wa kilomita 0.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba I yenye majira - nukta 381428MS, 9667684KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS880 MS kwa umbali wa kilomita 1.2 hadi ulipoanzia”

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to
To the top