Amri ya Kupanga Eneo la Nyantorotoro ya Mwaka 2023

Government Notice 324 of 2023

Amri ya Kupanga Eneo la Nyantorotoro ya Mwaka 2023
Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.

Tanzania
Town and Country Planning Act

Amri ya Kupanga Eneo la Nyantorotoro ya Mwaka 2023

Tangazo la Serikali 324 ya 2023

[Sura ya 355; Imetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1)]

1. Jina

Amri hii itajulikana kama Amri ya Kupanga Eneo la Nyantorotoro ya Mwaka 2023.

2. Utangazaji wa eneo la upangaji

Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji kwa madhumuni ya Sheria ya Mipangomiji.[Sura ya 355]

3. Mpango wa jumla na kina wa eneo

Mipango ya jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Geita.

Jedwali (limetengenezwa chini ya aya ya 2)

Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo—“Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 414975MS, 9677697KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa 82o kwa umbali wa kilometa 0.88 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 414467MS, 9678420KS; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa 158o kwa umbali wa kilometa 1.48 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba C yenye majira - nukta 413221MS, 9679216KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa 94o kwa umbali wa kilometa 1.36 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta 414054MS, 9677231KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa 81o kwa umbali wa kilometa 1.88 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majiranukta 415036MS, 9677697KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa 125o kwa umbali wa kilometa 1 hadi ulipoanzia”

History of this document

28 April 2023 this version
17 March 2023
Assented to
To the top