Collections
Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.
Tanzania
Criminal Procedure Act
Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka, 2025
Tangazo la Serikali 430 ya 2025
- Imechapishwa katika Subsidiary Legislation Supplement kwa 11 Julai 2025
- Imeidhinishwa tarehe 10 Julai 2025
- Ilianza tarehe 11 Julai 2025
- [Hili ni toleo la hati hii kutoka 11 Julai 2025.]
Sehemu ya kwanza – Masharti ya utangulizi
1. Jina
Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025.2. Matumizi
Kanuni hizi zitatumika kwa mashahidi kama walivyotafsiriwa katika Kanuni hizi.3. Tafsiri
Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—“amri ya ulinzi” maana yake ni amri ya mahakama inayoelekeza ulinzi wa shahidi;“kihatarishi” maana yake ni uwezekano wa kutokea kwa tishio au hatari;“kizimba maalum cha shahidi” maana yake ni sehemu ya kusimama au kukaa wakati wa kutoa ushahidi iliyoandaliwa mahsusi ili kumwezesha shahidi anayelindwa kutoa ushahidi bila kuonekana isipokuwa kwa jaji au hakimu anaeyeendesha shauri husika;“mahakama” maana yake ni mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza shauri ambalo amri ya ulinzi imeombwa;“mahakama ya chini” maana yake ni mahakama ya wilaya au mahakama ya hakimu mkazi;“mkutano kwa njia ya simu” maana yake ni utoaji wa ushahidi mahakamani kwa njia ya sauti kupitia simu au kifaa kingine cha mawasiliano;“mkutano kwa njia ya video” maana yake ni utoaji wa ushahidi mahakamani kwa njia ya video na sauti;“mtoto” maana yake ni mtu ambaye hajafikisha umri wa miaka kumi na nane;“shahidi” maana yake ni mtu anayehitaji ulinzi kutokana na tishio au hatari iliyopo au inayoweza kutokea kutokana na kutoa taarifa katika chombo cha kusimamia sheria, kutoa au kukubali kutoa ushahidi kuhusiana na kosa au shauri la jinai au kwa sababu nyingine yoyote ambayo mahakama inaweza kuona kuwa inatosheleza, na anajumuisha mtu anayestahili ulinzi kwa sababu ya kuwa na uhusiano na mtu huyo;“shahidi anayelindwa” maana yake ni shahidi aliye chini ya amri ya ulinzi;[Sura ya 20]“Sheria” maana yake ni Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai;“tishio” maana yake ni uwezekano wa matokeo mabaya kwa shahidi kutokana na kutoa ushahidi katika shauri na inajumuisha hatari yoyote ya kimwili au kisaikolojia, inayoweza kutokea kutokana na kushiriki kwake katika shauri hilo;“uhariri” inamaanisha kuondoa taarifa za utambulisho kutoka kwenye hati au kitu;“ulinzi wa shahidi” maana yake ni hatua au mbinu za kumlinda shahidi ambaye maisha, usalama, au mali yake inaweza kuwa katika hatari au tishio kutokana na kukubali kutoa ushahidi mahakamani katika shauri husika;“vifaa saidizi vya mawasiliano” maana yake ni vifaa au mbinu yoyote inayoweza kumwezesha shahidi kuwasiliana kwa ufanisi wakati wa kutoa ushahidi mahakamani.Sehemu ya pili – Ulinzi wa mashahidi
4. Maombi ya amri ya ulinzi
5. Mamlaka ya mahakama kutoa amri ya ulinzi wa shahidi
6. Amri za ulinzi
7. Ukomo wa amri ya ulinzi na athari zake
8. Mabadiliko ya amri ya ulinzi
Amri ya ulinzi inaweza kufutwa au kubadilishwa na mahakama kwa utashi wake au kufuatia maombi ikiwa itaridhika kuwa kuna mabadiliko ya hali ya shahidi tangu kutolewa kwa amri hiyo ambayo yanalazimisha mabadiliko ya amri ya ulinzi.9. Usikilizwaji wa faragha
10. Wajibu wa mahakama wakati wa kuhojiwa kwa shahidi na kupokelewa kwa vielelezo
Endapo usikilizaji wa shauri unahusisha shahidi aliye chini ya amri ya ulinzi, jaji au hakimu anayesikiliza shauri, atafanya yafuatayo:History of this document
11 July 2025 this version
10 July 2025
Assented to