Ask AI
Ask questions and understand this document faster using AI.
Tanzania
Labour Institutions Act
Kanuni za Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri ya Usuluhishi na Uamuzi za Mwaka, 2025
Tangazo la Serikali 61 ya 2025
- Imechapishwa katika Tanzania Government Gazette 5 hadi 31 Januari 2025
- Imeidhinishwa tarehe 27 Disemba 2024
- Ilianza tarehe 31 Januari 2025
- [Hili ni toleo la hati hii kutoka 31 Januari 2025.]
Sehemu ya kwanza – Masharti ya utangulizi
1. Jina
Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri ya Usuluhishi na Uamuzi za Mwaka 2025.2. Matumizi
Kanuni hizi zitatumika katika mwenendo wa mashauri yote katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.3. Tafsiri
Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo—“dawati la usaidizi wa huduma” maana yake ni dawati la usaidizi wa huduma lililoanzishwa chini ya Kanuni hizi;“mdaawa” maana yake ni mhusika yeyote katika shauri lililo mbele ya Tume;“mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri” maana yake ni mfumo wa kielektroniki wa usajili, uwasilishaji nyaraka na usikilizaji wa mashauri ulioanzishwa chini ya Kanuni hizi;“Mkurugenzi” maana yake ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi;“mkutano wa simu” maana yake ni mawasiliano ya moja kwa moja ya sauti kupitia simu au kifaa chochote cha mawasiliano kinachofanana na simu;“mkutano wa video” maana yake ni mkutano wa mtandaoni unaoendeshwa na Tume kwa kutumia teknolojia ya video na sauti ambapo Tume huendesha shauri kwa kusikiliza sauti inayoambatana na muonekano wa sura za wahusika walio mbali;“mtumiaji” maana yake ni mtumiaji aliyesajiliwa au mtumiaji aliyeidhinishwa na kusajiliwa na mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri;“mtumiaji aliyeidhinishwa” maana yake ni mshirika, mkurugenzi, mhusika, afisa au mfanyakazi ambaye ameteuliwa kama mtumiaji aliyeidhinishwa, na inaweza pia kujumuisha mwajiri, chama cha wafanyakazi au mwakilishi anayetambulika kisheria;“mtumiaji aliyesajiliwa” maana yake ni mtu binafsi au taasisi iliyopewa jina la mtumiaji na nywila iliyoidhinishwa na Tume kuufikia na kuutumia mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri;“mwangalizi” maana yake ni mtu yeyote ambaye anahudhuria shauri, lakini hana jukumu lolote katika shauri hilo;“msaidizi wa usikilizaji wa mbali wa mashauri” maana yake ni mtu aliyeteuliwa chini ya kanuni ya 37 kusaidia Tume na wahusika katika kuendesha mashauri ya mbali;“saini ya kielektroniki” ina maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Miamala ya Kielektroniki;[Sura ya 442]“saini salama ya kielektroniki” maana yake ni saini inayotambuliwa hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Miamala ya Kielektroniki;[Suya ya 442]“Sheria” maana yake ni Sheria ya Taasisi za Kazi;[Sura ya 300]“Tume” maana yake ni Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria na itajumuisha mtu au chombo chochote kilichoteuliwa na Tume kutekeleza majukumu ya Tume kwa mujibu wa Kanuni hizi; na“utambulisho wa mtumiaji” maana yake ni anwani ya barua pepe iliyotolewa au msimbo wa utambulisho uliotolewa wakati wa usajili ambao hutumiwa kuingia kwenye mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri.Sehemu ya pili – Huduma za usajili kwa njia ya kielektroniki
4. Kuanzishwa kwa mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri
5. Usimamizi wa utoaji huduma ya usajili wa mashauri kielektroniki
Huduma ya kufungua jalada kwa njia ya kielektroniki itakuwa chini ya usimamizi wa Tume.6. Kuanzishwa kwa dawati la usaidizi wa huduma
7. Mtumiaji aliyesajiliwa na mtumiaji aliyeidhinishwa
Sehemu ya tatu – Utaratibu wausajili wanyaraka kieletroniki
8. Nyaraka zinazosajiliwa kielektroniki
Mgogoro, maombi, nyaraka za malalamiko na nyaraka nyinginezo zozote zitawasilishwa kwa kuzingatia Kanuni hizi.9. Kumbukumbu rasmi za Tume
Kumbukumbu rasmi za Tume zitakuwa ni jalada la Shauri la kielektroniki, mwenendo unaohusu shauri hilo pamoja na nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa kwa njia isiyo ya kielektroniki.10. Utaratibu wa kusajili shauri kielektroniki
11. Maandalizi na muundo wa nyaraka
12. Kubadilisha nyaraka kuwa katika umbizo la hati kubebeka
13. Kusainiwa kwa nyaraka za kielektroniki
14. Hati za kiapo katika fomu ya kielektroniki
15. Utumaji nyaraka
16. Utunzaji wa nyaraka halisi
Nyaraka zote zilizowasilishwa kielektroniki, zitatunzwa kwa kuzingatia taratibu na muda uliowekwa kwenye Jedwali la utunzaji na utupaji nyaraka lililo chini ya Sheria ya Usimamizi na Uhifadhi wa Kumbukumbu na Nyaraka na zitatolewa kwa Tume wakati wowote zitakapohitajika.[Sura ya 309]17. Wajibu wa kutoa nyaraka halisi
Mdaawa ambaye amewasilisha nyaraka za kielektroniki atawajibika kutoa nyaraka halisi na kuthibitisha uhalisi wake.18. Utofauti
Pale ambapo nyaraka iliwasilishwa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri na kuna utofauti kati ya taarifa iliyoingia kwenye fomu ya uwasilishaji wa kielektroniki na taarifa iliyomo kwenye nyaraka, taarifa zilizomo katika nyaraka zitazingatiwa.19. Upatikanaji wa nyaraka za kielektroniki
Nyaraka zilizowasilishwa kwa njia ya kielektroniki katika shauri, zitatolewa kwa wadaawa, mawakili wao au wawakilishi walioidhinishwa, baada ya kutuma maombi kwa Tume pamoja na diski za kuhifadhia data au kifaa kingine chochote cha kumbukumbu cha mfumo wa kompyuta.20. Ruhusa ya kutosajli shauri kielektroniki
21. Tarehe na muda wa kuwasilisha nyaraka
22. Kuhesabu tarehe na muda wa kutuma nyaraka
Nyaraka iliyosajiliwa, kutumwa, kupokelewa au kuwasilishwa kwa Tume kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri na kukubaliwa na Tume, itachukuliwa kuwa imesajiliwa, imetumwa, imepokelewa au kuwasilishwa—23. Muda wa kutuma nyaraka unapoanza kuhesabiwa
24. Ukokotoaji wa muda
25. Matumizi ya nakala ngumu za maombi na nyaraka nyingine zilizowasilishwa kielektroniki
Nakala ngumu za maombi yote na nyaraka nyingine zilizowasilishwa kielektroniki zinaweza kuchapishwa na—26. Kuzipa majina nyaraka zinazowasilishwa kielektroniki
Nyaraka zote zinazowasilishwa kielektroniki zitapewa majina kwa namna sawa na nyaraka zinazowasilishwa kwa njia isiyo ya kielektroniki.27. Utunzaji na upatikanaji wa nyaraka zilizowasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri
Sehemu ya nne – Akaunti na taarifa kwa mtumiaji
28. Utambulisho wa mtumiaji
Anwani ya barua pepe iliyotolewa au msimbo wa utambulisho uliotolewa wakati wa usajili utatumika kama utambulisho wa kipekee wa mtumiaji.29. Kustahiki na usajili
30. Nywila ya mtumiaji
Wakati wa usajili, mtumiaji ataweka nywila ya kipekee kwa mujibu wa vigezo vilivyotolewa na mfumo na anaweza kubadilisha nywila yake wakati wowote.31. Usiri wa utambulisho wa mtumiaji na nywila
32. Akaunti nyingi za watumiaji
Mtumiaji au mtumiaji aliyeidhinishwa anaweza kufungua akaunti tofauti kwa kutumia anwani tofauti za barua pepe na atafuatilia kila akaunti na kuwasilisha nyaraka kwa usahihi.33. Upokeaji wa taarifa
34. Malipo ya ada
Ada zitalipwa kwa njia ya kielektroniki kwa kuzingatia taratibu na mfumo unaotumika kwa malipo ya Serikali.Sehemu ya tano – Usikilizaji wa mbaliwa mashauri
35. Mashauri ya mbali
36. Mazingira ya Tume kuelekeza usikilizwaji wa shauri kwa mbali
37. Uteuzi wa msaidizi wa usikilizaji wa mbali wa shauri
38. Kazi za msaidizi wa usikilizaji wa mbali wa shauri
Msaidizi wa usikilizaji wa mbali wa shauri atakuwa na kazi zifuatazo:39. Waangalizi
40. Utaratibu wa usikilizaji wa mbali wa mashauri
41. Zuio la kurekodi, nk., mwenendo wa shauri
Mwenendo wa shauri hautarekodiwa, kuchapishwa au kutangazwa kwa njia au namna yoyote na wadaawa au mtu mwingine yeyote isipokuwa kwa ruhusa ya Tume.42. Rejea kwa maamuzi mbalimbali
Endapo, katika usikilizaji wa mbali wa shauri, mdaawa anataka kurejea uamuzi uliotolewa katika shauri lolote ambalo haijaripotiwa au kufanya nukuu kutoka kwenye kitabu chochote au mamlaka nyingine yoyote ambayo sheria na utendaji unamtaka atoe nakala yake katika Tume, atatayarisha nyaraka iliyoorodheshwa na kifurushi cha kielektroniki cha mamlaka zilizotajwa na kuwasilisha kwa Tume kupitia mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri au njia nyingine yoyote ambayo Tume inaweza kuamuru na zitatolewa kwa wadaawa wengine wote au wawakilishi wao kabla ya shauri.43. Utoaji wa nyaraka
44. Utoaji wa vielelezo au maonesho halisi
45. Kuahirishwa kwa shauri
46. Kuahirishwa kwa mwenendo wa shauri kwa sababu mbalimbali
Endapo Tume imeelekeza usikilizaji wa mbali wa shauri uendelee na wakati wa usikilizaji ikabainika kuwa shauri la mbali au njia iliyochaguliwa—Sehemu ya sita – Masharti mbalimbali
47. Kurekodi na kutunza kumbukumbu za mwenendo wa mashauri ya Tume
48. Ombi la nakala ya mwenendo wa shauri uliorekodiwa
49. Kumbukumbu rasmi za Tume
50. Kusaini na kugonga muhuri kumbukumbu za Tume
51. Saini za kielektroniki kuwa na nguvu sawa na saini isiyo ya kielektroniki
Tuzo yoyote, uamuzi mdogo, amri, taarifa au wito wowote uliotiwa saini kielektroniki utakuwa na nguvu sawa kama Tume ingeweka saini yake kwenye nakala ya karatasi ya amri hiyo na kuweka kwenye rekodi kwa njia ya kawaida.History of this document
31 January 2025 this version
27 December 2024
Assented to